Naomba ushauri

Escoba vitu vingine ni vyakupotezea tu, haina sababu ya kukuumiza kichwa namna hiyo.
Mueleweshe Bf wako vizuri kwamba huyo sio mpenzi wako na hauna uhusiano naye, kama Bf wako ni mwelewa nadhani atakuelewa.

Mkanye huyo mwalimu mwenzio aache kabisa hiyo tabia yake, ikiwezekana badilisheni line za simu ili kufutilia mbali usumbufu usio na sababu.
 
Kabla hujaongea fikiria inaweza kubadili mtazamo wako na kabla hujahukumu fikiria ili utoe hukumu ya haki. kumhukumu mtu kabla hujamsikiliza vizuri sio kumtendea haki. mhusika halalamiki kutongozwa bali tabia ya kulazimishwa hadi kupelekea kuhatarisha uhusiano wake wa sasa.

Dada cha msingi ongea na bf wako kama ni muelewa atakuelewa kisha kaa naye mjadiliane cha kufanya kuhusu kumwadibisha huyo mwl.
 
walimu wa siku hizi hawana tofauti na wanafunzi wao kitabia
 

Nafikiri ingependeza sana hii thread ungetupia jukwaa la mahusiano, mapenzi urafiki, mbona kama siyo mahala pake humu au linaathari fulani kiataaluma na kwa elimu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…