Naomba ushauri

Naomba ushauri

Escoba vitu vingine ni vyakupotezea tu, haina sababu ya kukuumiza kichwa namna hiyo.
Mueleweshe Bf wako vizuri kwamba huyo sio mpenzi wako na hauna uhusiano naye, kama Bf wako ni mwelewa nadhani atakuelewa.

Mkanye huyo mwalimu mwenzio aache kabisa hiyo tabia yake, ikiwezekana badilisheni line za simu ili kufutilia mbali usumbufu usio na sababu.
 
Kabla hujaongea fikiria inaweza kubadili mtazamo wako na kabla hujahukumu fikiria ili utoe hukumu ya haki. kumhukumu mtu kabla hujamsikiliza vizuri sio kumtendea haki. mhusika halalamiki kutongozwa bali tabia ya kulazimishwa hadi kupelekea kuhatarisha uhusiano wake wa sasa.

Dada cha msingi ongea na bf wako kama ni muelewa atakuelewa kisha kaa naye mjadiliane cha kufanya kuhusu kumwadibisha huyo mwl.
 
walimu wa siku hizi hawana tofauti na wanafunzi wao kitabia
 
Kuna mwalimu nafundisha nae wa kiume anaitwa ( ) tunafundisha shule ya msingi () ipo Tarime , Mara. Alinitongoza nkamkataa, juzi boyfriend angu alipiga simu yeye akapokea , simu ilikua kwa chaji kwa mwalimu mwenzangu, akaanza kujibizana na boyfriend angu akamwambia eti yeye ( ) ndo ananichukua kwa sasa. Alichkua pia namba ya boyfriend angu akawa anampigia simu na anatuma text kwake kwamba mi nam cheat. Sasa hv nipo dar na boyfriend angu ananitumia msg et kwann cpokea simu ake pia katuma text kwa bf angu anamwambia niwashe simu. hivi mtu kama huyu nimfanyanyaje ? naomba ushauri hata wa kisheria . Juzi nilimwambia mwalimu mkuu tukamwekea kikao akamuonya na yeye akasema hatonisumbua sasa naona anaendelea mi nikiwa na bf. ushauri pls

Nafikiri ingependeza sana hii thread ungetupia jukwaa la mahusiano, mapenzi urafiki, mbona kama siyo mahala pake humu au linaathari fulani kiataaluma na kwa elimu?
 
Back
Top Bottom