Wana Jf! Ni miezi sita tangu nianze kupata maumivu kwenye kichwa cha uume.nimetumia dawa kwa ushauri wa daktar wakidai ni UTI Baada ya kufanya cultural sensitivity pale KCMC.dozi ya mwisho niliyotumia inaitwa clindamycn 450/7: Lakini bado napata maumivu. Nimerudi hosp Urology nikamuona daktar baada ya kumueleza historia ya ugonjwa akasema hawezi kunipa dawa hadi nipate kipimo kinaitwa DOPPLER ULTTRASOUND. Balaa lilianzia hapo nilikuta mashine ina wiki mbili haifanyi kazi hadi leo hii. Naomba ushauri na jinsi ya kupata hicho kipimo Moshi na Arusha au nitakavyosaidika.