Naomba utaratibu wa kuwasilisha malalamiko

Los técnicos

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2014
Posts
3,012
Reaction score
2,637
Husika na mada tajwa hapo juu ningependa kujua kutoka kwa wabobezi wa sheria juu ya;

1. Utaratibu upi uanaotakiwa kufuatwa pale mashitaka yanapofutwa kwa kigezo cha mlalamikaji kutohudhulia mahakamani bila ya mlalamikaji kupewa taarifa ya mahala na muda wa kesi kusikilizwa?

2.utaratibu juu ya kuomba nakala ya hukumu
 
Kesi ikifutwa kwa mlalamikaji kutoenda mahakamani (lack of prosecution) hatua ya kuchukua ni kuiomba mahakama iliyofuta hiyo kesi kuirudisha (restoration) ili iweze kusikilizwa kwny misingi (on merits) sheria inayotumika kuomba maombi hayo inategeme na kesi hyo ipo mahakama/baraza gani la kutoa haki. NB USIKATE RUFAA TAFADHARI. (Costs zitafolllow event)

Lakini utakachopaswa kuishawishi mahakama ni sababu iliyokufanya USHINDWE kuhudhuria mahakamani hadi kesi ikafutwa. Na kwa sababu hyo umenyimwa haki wa kusikilizwa ( the right to be heard)

Mwone mwanasheria alie karb nawe kwa kuandikiwa hati ya maombi na ushauri kwan yy ataona nyaraka zako na kujiridhishwa zaidi.
 
Ahsante sana kwa response yako.
Lakini vipi unaweza kuiomba mahakama kuirudisha kesi.
 
Ndiyo inawezekana na ndo utaratibu siku zote, had pale sheria zitakapotamka vinginevyo. Kwan kesi ilikuwa mahakama gani???
 
Ahsante sana kwa response yako.
Lakini vipi unaweza kuiomba mahakama kuirudisha kesi.
Na vipi kuhusu utaratibu wa kurudisha kesi yaani hiyo (restoration) unaandika barua au inakuwaje? Na muda wa kufanya hivyo?
 
Na vipi kuhusu utaratibu wa kurudisha kesi yaani hiyo (restoration) unaandika barua au inakuwaje? Na muda wa kufanya hivyo?
Unaandika "chamber summons" na "Affidavit" yake sio BARUA mkuu!. Na unaonesha unaomba maombi yko chini ya kifungu gan (Non citation render ur application dismissed). Kwa kuwa ni mahakama ya wilaya sheria inayotumika ni CPC (under r. IX ).

Muda wa kuomba ni 30dys from the date of dismisal order.

NB: wewe ni lawyer unataka idea sharing ama hujui lolote about Law??? Coz unavyoniuliza ni km unajua kitu fulan unatega kujiridhisha. Halaf nimeandika maneno ya profession ya sheria ndo maana nimekuuliza wewe ni Lawyer???
 
Hapana mimi si lawyer ila nili "quote' neno restoration kutoka kwenye maelezo yako I 'm ignorant of law judicial matters.
 
Nimkukubali MKUU , naomba nisaidie hill nijue ninaanzia WAP, nilinunua kiwanja sehemu ila kuna mgogoro jamaa alie niuzia na MTU mwingine ,wameenda mahakamani jamaa alie niuzia kashindwa kesi ,hii ni Mara ya pili kushindwa sasa huyu aliyeshindwa nimemwambia nimpatie PESA kakataa .na mm nimesha jenga tayari .Na mahakama haijaniambia chochote tangu nimeanza ujenzi hadi sasa NAOMBA Msaada.

Sent from my Z4 using JamiiForums mobile app
 
Una muda gan unaishi/unapamiliki hapo?? (Muhimu)

Wewe ni "bonafide purchaser" but ktika mauziano yenu either kulikuwa na "fraud" or "misrepresentation" ya huyo mtu aliekuuzia. So kafungue kesi ya madai dhidi ya huyo mtu (aliekuuzia) ukidai pesa yako ya kuuziana kiwanja na gharama za kuendeleza kiwanja hicho (wewe co trespasser/mvamizi) so unasitahili kurudishiwa gharama zako.

Kwa kuwa ulikuwa ni mkataba....mkataba unapovunjika ama kama unaweza kubatilishwa (voidable) pande zote za mkataba hurudi km mwanzo ambapo mkataba haukuwepo (i.e resititution) the aim of breach of contract is for "resititution" the party suffered. So wewe hutakiwi kupoteza bali kurudishiwa gharama zako.
 
Ndiyo inawezekana na ndo utaratibu siku zote, had pale sheria zitakapotamka vinginevyo. Kwan kesi ilikuwa mahakama gani???
Habari za mida wadau?
Kuhusu ufutwaji wa ile jinai kwa mlalamikaji kutohudhuria msaada wa kisheria tulioupata maeneo ya karibu unadai kwa jinsi kesi ilivyokuwa framed mshitaki ni jamhuri
Sasa kwa mazingira hayo kuiomba kesi kurudishwa mahakamani kuna changamoto moja maana PP mpelelezi wa kesi ofisi inasema kasafiri na aliye isimamia anadai tumsubiri mhusika.
Lakini nijuavyo ofisi huwa haisafiri na muda unaisha msaada nini cha kufanya wadau

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…