Naomba wakristo tuungane kumpinga mchungaji Masisi

Naomba wakristo tuungane kumpinga mchungaji Masisi

mandawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
772
Reaction score
1,119
Mimi kama Kristo niliolelewa nikijua Biblia ni kitabu kitakatifu, nimesikitishwa sana na huyu mchungaji Masisi kwa makufuru yake kuhusu Biblia.

Masisi hana tofauti na wakristo wengi ambao tumekuzwa tukielewa Biblia ni neo la kweli la Mungu, ila kiburi anachokionyesha sijui kwa usomi wa kujiita Dr. anaona ni rahisi kupotosha Umma wa wakristu.

Nashukuru Serikali kwa kulisimamisha kanisa, ila kwangu mimi naona sisi kama wakristo tuuungane kupinga kila kitu anachfanya pamoja na product yao ya Zoa Zoa. Maana naona kabisa huyu ni agent wa Kuzimu, hivyo sio vema kujihusisha nae kwa chochote kinachomuhusu. Wakristo Tuwe macho sana nyakati hizi, tusome neno kwa bidii, tuzijue hila za mwovu.

Kuacha wasomi wa theorojia watuhubirie kila siku ..matokeo ndio hayo ya upotoshaji..... Masisi acha kiburi.

Pia soma > Serikali yalifungia kanisa la Spirit Word Ministry

Huyu na yule mpambe wake anaosifia pombe na kukataa fungu la kumi Bora hata zumaridi
 
Hawa ndo manabii wa uongo tuliombiwa.Kupinga mafundisho ya Paulo ni kupinga Ukristu,Paulo amendika karibia nusu ya vitabu vyote vya agano jipya. Kutokukubaliana naye means unapinga ukristu wote. Christianity as we know today is structured through Paul teachings.

Akimaliza atoe sasa maelekezo tutumiee kitabu gani?au tumsikilize nani? Huyu ameanza kuchanganyikiwa.
 
Nimemsikiliza Jamaa anasema amri kumi za Mungu ni Ushenzi na upuuzi,anasema,wao ni kizazi cha Kristo hawafungwi na amri kumi za Mungu.

Anamuita Paulo ni Mjinga mmoja na angekuepo yeye enzi zake angemkea na kumwambia acha upotoshaji

Pamoja na kwamba kuna Uhuru wa kuabudu ila ukifuata mafundisho yake huyu uwe na uhakika unaenda kupotea.
 
Uhuru wa kuabudu usiingiliwe, kama anakuudhi ya nini kumsikiliza?
 
Huyu labda katumwa na waislam jamii ya yemen kuleta havoc na commotions za kiimani
 
Msihangaike na wangese kama hao.
Yanini upoteze muda na bando lako kusikiliza ukhanithi wake.
Ahubirie wajinga wenzake.
 
Hapa utata tena! kwahiyo yeye Mungu anayemuongelea hapa kamjua kupitia akina nani?(sio kwamba kasoma ujumbe wa hao mitume ndio kamjua Mungu)

Anajaribu kusema biblia ina madhaifu,sasa ikiwa ina mapungufu yeye kwanini anatumia kitabu chenye madhaifu kuendelea kupotosha waumini wake?kwanini asitumie hicho kitabu kilichokuwa sawa kufundisha yaliyokuwa sahihi?

Mtume Paulo maisha yake kabla yakupewa ujumbe na Mungu yalijawa na changamoto nyingi lakini hilo halijawahi kuwa jambo kwa mkristo maana siku zote kinachoangaliwa ni ujumbe(ujumbe wenye kumfanya mwanadamu atambue mwanga na giza na aishi katika misingi mizuri) na umetoka kwa nani basi.
 
Ni mawazo yake, pingana nae hoja. Mimi naweza kusema "ukristu ni biashara" sasa pingana nami kwa hoja, ukiniona ni mjinga NAMI nakuita "zuzu kwa kupokea imani bila ya kuhoji ".
 
Back
Top Bottom