Naomba wasifu wa gari aina ya Toyota Rush

Naomba wasifu wa gari aina ya Toyota Rush

Yes, rush ni model ya pili ya Toyota Cami/Daihatsu Terios. Ingawa Daihatsu ni kampuni inayomilikiwa (subsidiary) na Toyota Motors Corporation, so basically ni Toyota tu. Ila Kiuhalisia, huwa sipendi saana magari yanayotengenezwa na subsidiary companies za makampuni makubwa. Sometimes zinakua na usumbufu kidogo, hasa kwenye spare parts.

So, Rush ni gari nzuri, good ground clearance, higher visibility, na zipo zenye AWD/4WD, ila ni a bit expensive, sababu ni gari ya karibuni. Ila wa comparison, I'd rather have a RAV4 instead. Hata ile model ya kwanza.
Nilikuwa natamani sana kumiliki Toyota Rush ila baada ya kautafiti ka muda nikaamua kuagiza Toyota Rav4!
 
Hongera sana mkuu kwa hiyo ni gari moja ya kisure
Mkuu kuwa ya kisure au ya kawaida nafikiri inategemea sana mfuko wa mtu. Kwa upande wangu mimi ningependelea gari kutoka kwa main manufacturer kuliko subsidiary. Pili ukiangalia size ya engine ni ndogo kwa hiyo kama budget in tight ni nzuri. Kisha gari ambazo ni high end huwa si front wheel drive kwa sababu ya power na engine size. Front wheel unaweza kuwa na engine kama V6,inline 4 lakini engines kama inline 6 na V8 etc etc mara nyingi huwezi kukuta front wheel drive na magari huwa bei yake ni ya juu na yanakuwa na daraja tofauti na Daihatsu Terio etc etc.
 
Nilikuwa natamani sana kumiliki Toyota Rush ila baada ya kautafiti ka muda nikaamua kuagiza Toyota Rav4!
Kwa hilo nakuunga mkia. Kama alivyosema mkuu Rugambwa hapo juu,nafikiri ni bora kununua kwa main manufacturer kuliko subsidiary.
 
toyota rush ni sawa kabisa na toyota passo au na daihatsu terrios kwenye engine hata gearbox hata control box ni sawasawa kabisaa tofauti body tuu.mfano engine ya rush ni 3SZ VE ni sawa sawa na K3 ya passo na terrious gearbox pia ni sawa sawa na control box ya rush na transmission control ni sawa kabisa na ya passo pia.
 
mmenikumbusha mwaka 2010 kuna.mtu alinunua toyota cami sa siku moja nimepanda nkackia wakiongelea kuhusu service.....mwenye gari akasema hii sio toyota kabisa nkashangaa sema sikuuliza kwann sio toyota na kila kitu kinaonekana ni toyota
 
Nami nichangie kidogo. Kwanza ni kweli RUSH ni Cami/Terious second Generation. Pia ni kweli engine yake ni 1.5L hasa. Hii maana yake ni sawa na carina Ti, baadhi ya IST, Raum new model, Runx, Alex na zingine zenye cc ndogo ambazo ni VVTI. Advantage kubwa kwa Rush ni kuwa iko juu na nyingi ni 4WD na kwa hiyo inapita pale linapopita RAV4.Kwa hiyo kwa suala la mafuta, ipo tofauti kubwa sana kati ya RAV lolote, kuanzia Old Model, Kili time na New model.
Nashauri mtoa mada achukue Rush badala ya RAV4 kama anataka economy but still comfortable and compact.
Lakini kama uko kwenye mji usio na folen, nunua RAV lolote.
Kweli kabisa.
 
Mkuu naomba nichangie kidogo kuhusu hiyo gari. Kwanza naomba nikuambie kitu ambacho watu wengi huwa hawakifahamu au kukifuatilia. Kinaitwa badge engineering. Yaani kampuni moja inatengeza kifaa kwa makubaliano na kampuni nyinge kisha wana stamp jina na badge. Hiyo Toyoya Rush sio Toyota ni Daihatsu Terios second generation.Si Toyota tu na Daihatsu ndo wanafanya hivyo,hata kampuni nyingine kama Nissana alikuwa ananunua gari ndogo kwa kampuni ngodo ndogo kama mitsubishi (Ingawa kwa sasa Nissana alimnunua Mitsubishi baada ya fuel ecomony scandal)
Engine yake ni options mbili 1.3L au 1.5L. Ni engines ndogo sana kwa hiyo ulaji wa mafuta nadhani utakuwa mzuri. Sina uzoefu kuhusu upatikanaji wa vifaa huko nyumbani.
Nafikiri nimekupa mwanga kidogo ndugu yangu.

Hujui kama daihatsu na Lexus ni kampuni Dada za Toyota
 
Hujui kama daihatsu na Lexus ni kampuni Dada za Toyota
Sio kwamba sijui,na kama ukisoma hiyo post vizuri na post nyinginezo kama za Mkuu Rugambwa utaona kabisa hilo jambo nalifahamu vizuri sana.
 
Ahsanteni sana wakuu.nimefaidika sana na post zenu
 
Sidhani kama spea zake ziko widely available!...ila mm magari ya new edition huwa nayaogopa...maana kakizima tu........
 
Hii gari ni nzuri tatizo lipo kwenye kodi waliyo iwekea kodi yake ni kichaaa gari kodi milion 11 wakati hiyo kodi unaweza kununua toyota IST
 
mmenikumbusha mwaka 2010 kuna.mtu alinunua toyota cami sa siku moja nimepanda nkackia wakiongelea kuhusu service.....mwenye gari akasema hii sio toyota kabisa nkashangaa sema sikuuliza kwann sio toyota na kila kitu kinaonekana ni toyota
Hizo Cami zimejazana Garage tatizo spare hakuna, zimefunikwa na turubai
 
Back
Top Bottom