Naomba wataalamu wetu wanisaidie kutafsiri kipengele hiki katika lugha yetu ya Kiswahili

Sitatia siri za baraza la Mawaziri,na Makatibu Wakuu nao wanaapa hawatatoa siri za Serikali.

Hakuna mkataba wa Serikali unaweza ukawekwa wazi kiasi hicho,labda iwe Serikali ya Abunuasi
Tangu lini mkataba ukawa siri, mkuu? Which school did you go?
 
Dah mbona mkataba wa kimangungo huu?so state haina power ya kuvunja mkataba huu no Mara waah🤣🤣nacheka kama mazuri🤔
 
Kipengele hiki naambiwa kiko kwenye makubaliano kati ya Tanzania na Saudia kuhusu uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam.

View attachment 2648997
WOW!
Nawaomba wataalam wetu wa lugha wanisaidie kutafsiri hii katika lugha yetu ya taifa Kiswahili.
Ilete kwanza hiyo iliyotajwa hapo kama "Article 20 of this agteement".

Ili mtu aweze kutoa tafsri sahihi, lazima ajue kwanza article hiyo imesema nini
 
[emoji23][emoji1787]dah nimecheka
 
Kipengele hiki naambiwa kiko kwenye makubaliano kati ya Tanzania na Saudia kuhusu uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam. WOW!

View attachment 2648997


Nawaomba wataalam wetu wa lugha wanisaidie kutafsiri hii katika lugha yetu ya taifa Kiswahili.
Hakuna upande wowote ule kati ya mataifa yetu ambao utakuwa na haki ya kukanusha, kujiondoa, kusimamisha au kutengua mkataba huu kwa namna yoyote ile, ikiwemo tukio la ukiukaji, mabadiliko yalo na athari, uharibifu wa mahusiano ya kibalozi au uwakilishi, au visababishi vyovyote vinotambuliwa na sheria za kimataifa. Licha ya yalopita, ubishani wowote kati ya sehemu mbili za mkataba kwa kuzingatia mazingira hayo kutokukubaliana kokote kati ya sehemu hizi mbili za mkataba kutashughulikiwa kwa mujibu wa mahitaji ya sehemu ya 20 ya mkataba huu.

Cha msingi leta hiyo Article 20 tuichambue.
 
Hakuna mkataba wa Serikali unaweza ukawekwa wazi kiasi hicho,labda iwe Serikali ya Abunuasi
Inakuwa siri ya nani...serikali au wana CCM? Je Bandari ni ya nani...wananchi, serikali au wana CCM? Kumbuka hao uliowataja ni watumishi wa wananchi.
 
Thubutuuuu ulemavu wa ukubwani una utaka kwa nguvu mnooo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]


Basi na tukae kimya tutulie tunyolewe kama wendawazimu.
 
Sitatia siri za baraza la Mawaziri,na Makatibu Wakuu nao wanaapa hawatatoa siri za Serikali.

Hakuna mkataba wa Serikali unaweza ukawekwa wazi kiasi hicho,labda iwe Serikali ya Abunuasi
Ndio ujue kitu kiko mtaani now.
 
Wanasheria wetu wasomi na wabobezi wanasemaje kuhusu hili?
 
Labda mimi ndio niko nyuma na hizi Habari
Mkataba upi huo na bandari ipi?
Dubai sio Saudia au mnatoa bandari zote na wanagawana?
Next Oman na Kuwait labda
 
Maana yake ya kwanza ni kwamba kama kutatokea jambo lolote, wahusika watalishugjulikia kulingana Na utaratibu uliokubaliwa katika KIFUNGU CHA 20, na na sio kijitoa ama vinginevyo.
 
Kama mlikua mnatafuta sababu ya kuandamana/kukinukisha, hii ndo imejileta sasa mkizembea na hapa basi subirini kupigwa mnada. Natamani kujua hyo article 20 ya huo mkataba inasemaje kwenye utatuzi wa migongano, mwenye nayo pliz!
 
Mleta hoja tuwekee na hicho kifunga Cha 20 tu balance story
 
Hila hapa full Mangungo contract!
 
Aiseeeee !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…