Naomba watalaam wa pande zote Kenya na Tanzania musaidie. GDP inapatikanaje?

Naomba watalaam wa pande zote Kenya na Tanzania musaidie. GDP inapatikanaje?

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Salamu wa JF. Naomba matusi yasiwepo.

GDP (gross domestic product) inapatikanaje? Mpaka mashirika ya kimataifa wanatoa ripoti.

Kwa upande wangu nikichukulia neno domestic product inakuwa na maana ya mazao yatokanao na uzalishaji wa ndani.

Ninaomba kujua hao wataalamu wa mashirika ya kimataifa wanapataje data na kutoa ripoti?

Kwa mfano nikichukulia Tanzania, kuna products nyingi sana tunazalisha. Products hizo ukiziweka kwenye value ya pesa ni pesa nyingi mno.

Mf: Upande wa kilimo let say Tanzania mwaka huu imezalisha Tani 10,000,000 za mchele. Je, products hizi haziwezi kuwa converted to GDP?

Au wanaposema Domestic Product maana yake ni tafauti?

Ninaweza kuongeza tena mfano: Tanzania ipo na ujenzi wa SGR from own source kutokana na makusanyo ya kodi. Je, hayo hayawezi kuingizwa kwenye GDP!?

Vilevile mwaka 2015 makusanyo ya kodi toka TRA yalikuwa wastani wa Tsh800b kwa mwezi sasa hivi ni Tsh1.9T kwa mwezi je, hayo hayawezi kuingizwa kwenye GDP?

Mizigo imeongezeka badarini, na WFP wanapitisha na kununua chakula TZ. Hii imekaaje wajameni!?

Naomba tujadili kwa kina hii GDP inapatikanaje?
 
Tuanzie na per capita income ndipo twende kwenye GDP
Labda tungeeleweshana kwanza how GDP calculated!?

Maana nasikia per capita income ni GDP/Population.

Nadhani kile kitendawili cha GDP tukikitegua per capita itakuwa kama kusukuma mlevi.
 
Huyu GDP ni nini!?

Makusanyo upande wa madini yameongezeka lakini GDP ya Tanzania ipo palepale.

What is GDP!?

 
Huyu GDP ni nini!?
Makusanyo upande wa madini yameongezeka lakini GDP ya Tanzania ipo palepale.

What is GDP!?
GDP (Jumla ya Pato la Taifa) ni kipimo cha jumla ya pato la utajiri ambalo linapatikana ndani ya mipaka ya nchi katika muda maalumu. Kwa maneno mengine Pato la Taifa ni tathmini ya bidhaa zote na huduma ambazo zinaundwa na zinabadilishwa kwa fedha.

Kama jumla ya thamani ya bidhaa na huduma mwaka huu ni asilimia 1 zaidi kuliko ya mwaka jana basi ukuaji wa pato la utajiri ni asilimia 1. Lakini jumla ya pato la taifa (GDP) huacha kazi zingine za thamani ambazo zingeweza kujumuishwa – kwa mfano, uendeshaji wa kaya na familia kwa kupata nishati rahisi na maji, na pia watu kujenga nyumba zao kwa kutumia vifaa vya asilia na ustawishaji wa vyakula kwa ajili ya matumizi yao.

Kwa kifupi hivi ndivyo GDP hupatikana.
 
GDP (Jumla ya Pato la Taifa) ni kipimo cha jumla ya pato la utajiri ambalo linapatikana ndani ya mipaka ya nchi katika muda maalumu. Kwa maneno mengine Pato la Taifa ni tathmini ya bidhaa zote na huduma ambazo zinaundwa na zinabadilishwa kwa fedha.

Kama jumla ya thamani ya bidhaa na huduma mwaka huu ni asilimia 1 zaidi kuliko ya mwaka jana basi ukuaji wa pato la utajiri ni asilimia 1. Lakini jumla ya pato la taifa (GDP) huacha kazi zingine za thamani ambazo zingeweza kujumuishwa – kwa mfano, uendeshaji wa kaya na familia kwa kupata nishati rahisi na maji, na pia watu kujenga nyumba zao kwa kutumia vifaa vya asilia na ustawishaji wa vyakula kwa ajili ya matumizi yao...

Kwa kifupi hivi ndivyo GDP hupatikana...
Ninashukuru sana. Je, utalii nao ni bidhaa!?
Kama ni hivyo mwaka 2018 Tanzania ilipata mapato makubwa. Lakini GDP haikuongezeka why!?

Screenshot_20200611-074214.png
 
Venus Star,

Sawa kaa mkao wa kula tuende step by step. Kiswahili changu ni kibovu lakini hamna namna itabidi nikitumie hapa. Gdp kwa lugha ya yahe na hoipoloi ni kipimo cha kiwango cha uzalishaji wa mizigo na huduma yaani goods and services katika nchi kwa kipindi cha mwaka moja. Kila nchi huwa inazalisha mizigo na huduma kwa kiwango fulani. Jumla ya bei ya mizigo na huduma ambayo nchi husika inazalisha kwa kipindi cha mwaka moja ndio Gdp. Hii ndio definition rahisi. Kuna njia tatu za kucalculate Gdp lakini hio hatutaongea hapa.

Kwa hivyo, ukilima tani 10,000 ya mchele basi hiyo itawekwa kwenye Gdp. Sgr pia ni product yaani good (infrastructure) kwa hivyo value yake, wakati wa ujenzi, itawekwa kwenye Gdp. Hapo kwa mizigo ya Wfp bandarini, kama mizigo imezalishwa nje ya nchi na haitumiki kama malighafi ndani ya nchi bali ipo on transit (kwa mfano kuelekea Uganda,) basi hio haiwekwi kwenye Gdp
 
Ninashukuru sana. Je, utalii nao ni bidhaa!?
Kama ni hivyo mwaka 2018 Tanzania ilipata mapato makubwa. Lakini GDP haikuongezeka why!?

View attachment 1474695
Hapa kuna factors nyingi zinazoweza kufanya GDP ipande au isipande (mimi siyo mchumi, nadhani wachumi watatusaidia), kuna kitu kinaitwa Macroeconomic Stability (Uchumi Mkuu Imara) ambacho ni matokeo ya kuwa na kodi ya hazina, sera za fedha na kiwango cha kubadilishana fedha inayokusudia kufikia malengo ya uchumi mkuu kama vile ukuaji wa uchumi, kupanda kwa gharama za maisha, madeni ya nje na akiba halisi ya kimataifa. Lakini pia huwezi kuuacha Uchumi Mdogo (Microeconomics) ambao ni elimu kuhusu jinsi viwanda, sekta fulani, biashara au kaya zinavyofanya kazi.
 
Ukija kwenye Ukuaji Halisi wa uchumi, Kuna vipengele viwili: GDP na GNP (jumla ya Pato la Taifa likiongezea biashara ya ndani na biashara ya nje), kama ukuaji ni asilimia 7 kwa mwaka, lakini mfumuko wa bei umekuwa asilimia 5 basi Ukuaji Halisi unakuwa asilimia 2 tu kwa mwaka.
 
Sawa kaa mkao wa kula tuende step by step. Kiswahili changu ni kibovu lakini hamna namna itabidi nikitumie hapa. Gdp kwa lugha ya yahe na hoipoloi ni kipimo cha kiwango cha uzalishaji wa mizigo na huduma yaani goods and services katika nchi kwa kipindi cha mwaka moja. Kila nchi huwa inazalisha mizigo na huduma kwa kiwango fulani. Jumla ya bei ya mizigo na huduma ambayo nchi husika inazalisha kwa kipindi cha mwaka moja ndio Gdp. Hii ndio definition rahisi. Kuna njia tatu za kucalculate Gdp lakini hio hatutaongea hapa. Kwa hivyo, ukilima tani 10,000 ya mchele basi hiyo itawekwa kwenye Gdp. Sgr pia ni product yaani good (infrastructure) kwa hivyo value yake, wakati wa ujenzi, itawekwa kwenye Gdp. Hapo kwa mizigo ya Wfp bandarini, kama mizigo imezalishwa nje ya nchi na haitumiki kama malighafi ndani ya nchi bali ipo on transit (kwa mfano kuelekea Uganda,) basi hio haiwekwi kwenye Gdp
Asante sana nimekuelewa kwa kiasi fulani. Ni kukusahihisha kidogo tu. Usitumie neno mizigo tumia neno bidhaa
Goods = Bidhaa
Service = huduma

Asante sana.
 
Hapa kuna factors nyingi zinazoweza kufanya GDP ipande au isipande (mimi siyo mchumi, nadhani wachumi watatusaidia), kuna kitu kinaitwa Macroeconomic Stability (Uchumi Mkuu Imara) ambacho ni matokeo ya kuwa na kodi ya hazina, sera za fedha na kiwango cha kubadilishana fedha inayokusudia kufikia malengo ya uchumi mkuu kama vile ukuaji wa uchumi, kupanda kwa gharama za maisha, madeni ya nje na akiba halisi ya kimataifa. Lakini pia huwezi kuuacha Uchumi Mdogo (Microeconomics) ambao ni elimu kuhusu jinsi viwanda, sekta fulani, biashara au kaya zinavyofanya kazi.
Asante sana kwa majibu haya mazuri.

Naomba sasa kuchambua kitu kimoja kwenye kingine.

Hivyo vigezo vinafanya fanyaje GDP iongezeke!? Mwaka 2018 Tanzania ilikuwa inakuwa kwa 7+% mwaka 2019 ikakuwa kwa 6.8% lakini GDP haikuongezeka ilibaki pale pale.

How and why?
 
Nadhani unaweza kuchukua mfano niliotoa kwenye posti #10, ni kweli GDP ilishuka toka 7+% kwenda 6.8% lakini pia mfumuko wa bei ulipungua kwa takriban asilimia 1 na hivyo kufanya GDP ibaki ileile...
Duh!! Hapa pagumu sasa. Kwahiyo hapa unataka kuniambia mfumko wa bei kupanda unasababisha GDP ipande?

Samahani kwa hili.
 
Duh!! Hapa pagumu sasa. Kwahiyo hapa unataka kuniambia mfumko wa bei kupanda unasababisha GDP ipande!?

Samahani kwa hili.
Mfumuko wa Bei (Inflation) ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma mbalimbali, zinazotumiwa na sampuli wakilishi ya kaya binafsi katika nchi, zinazokusanywa kila mwezi katika kila mkoa. Sasa ukifuatilia kwa Tanzania utagundua kwa miaka miwili mfululizo haukupanda bali ulishuka, kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini Tanzania (NBS).

Kwa mfano, NBS wamefafanua kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi April,2020 umepungua hadi 3.3 % kutoka 3.4% kwa mwaka ulioishia Machi 2020.
 
Mfumuko wa Bei (Inflation) ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma mbalimbali, zinazotumiwa na sampuli wakilishi ya kaya binafsi katika nchi, zinazokusanywa kila mwezi katika kila mkoa. Sasa ukifuatilia kwa Tanzania utagundua kwa miaka miwili mfululizo haukupanda bali ulishuka, kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini Tanzania (NBS)...

Kwa mfano, NBS wamefafanua kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi April,2020 umepungua hadi 3.3 % kutoka 3.4% kwa mwaka ulioishia Machi 2020...
Bado ndugu swali langu hujalijinibu. Je, kupanda kwa kumfumuko wa bei unaongeza GDP!?
 
Bado ndugu swali langu hujalijinibu.
Je, kupanda kwa kumfumuko wa bei unaongeza GDP!?
Sijajua unataka nijibuje kwani nimejaribu kutoa mifano inayoonesha uhusiano kati ya mfumuko wa bei na Pato la Taifa. Labda nieleze hivi: ndiyo GDP inarekebishwa na mfumuko wa bei.
 
Bado ndugu swali langu hujalijinibu.
Je, kupanda kwa kumfumuko wa bei unaongeza GDP!?
Katika hoja yangu kwenye posti #14, naiona shaka yako kuhusu uhusiano kati ya mfumuko wa bei na Pato la Taifa. Wapo wachumi ambao huuangalia uhusiano wa ukuaji wa uchumi na mfumuko wa bei kwa kutumia nadharia ya quantity theory of money ambayo kimsingi inasema mfumuko wa bei hutokea pale fedha zinapoongezeka kwa kasi zaidi kuliko uzalishaji wa vitu halisi.

Katika nadharia hii ongezeko “sahihi” la ujazi wa fedha (m) linaweza kukokotolewa kama ifuatavyo: m = p + y endapo kasi ya mzunguko wa fedha (velocity of money circulation (v)) haibadiliki. Hii maana yake ni kwamba, ukuaji wa fedha (m) unapaswa kuwa sawa na mfumuko wa bei (p) jumlisha ukuaji halisi wa uchumi (y).

Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia kuwa mfumuko wa bei unaotumika katika kanuni hii siyo ule unaotokana na fahirisi ya bei ya walaji (consumer price index) bali ni ule unaotokana na fahirisi ya pato la taifa (GDP deflator). Kutokana na nadharia hii tunaweza kusema kuwa ukuaji wa uchumi ni sawa na tofauti kati ya ukuaji wa fedha na mfumuko wa bei...
 
Back
Top Bottom