Naomba watalaam wa pande zote Kenya na Tanzania musaidie. GDP inapatikanaje?

Naomba watalaam wa pande zote Kenya na Tanzania musaidie. GDP inapatikanaje?

GDP( GROSS DOMESTIC PRODUCT) Hii hujumlisha huduma na bidha zote zilizo zalishwa ndani ya nchi bila kujal aliye zalisha ni mzawa au mgeni lakin haita husisha bidha au huduma kutoka nje y nchi hatakam aliye zalisha huko nje ni mzawa.

GNP(GROSS NATIONAL PRODUCT) Hii hujumlisha bidha na huduma zote zinazo zalishwa ndani ya nchi na nje ya nchi ila na wazawa tu wa nchi husika, mfano wa Tz walio ndani ya nchi n wale walio nje..kwaiyo value za dhaman wanazo zalisha zita jumlishwa.
Fomular ya kupata GDP

GDP= C+I+G+(E-I) au
GDP=C+I+G+NX

Where by
C=consuption-matumizi ya kila siku kwenye huduma na bidha
I=investment-hapa ni uwekezaji unaofanywa ndani y nchi pia dhamani yke lzima ijumlishwe
G= goverment expenditure-matumizi yote ya serikali lazima ya jumlishwe kwenye ili kujua ukuwaj wa gdp
E=export-kile kinacho zalishwa ndani n kuzwa njee either ni biza au huduma
I=import nikile kinach zalishwa njee
NX= net export-ili kupata net export lzm ukuchuw kile chote kilicho zalishwa ndani utoe kile kilicho ingizwa kutok nje...then kitakach bakia utajumlisha kwenye hesabu

Lkn jua Tanzania ina sector nyingi zinazo ingiza hela ila hazija tambulika km formal sector kwaiyo huwa haziesabiwi kwenye gdp....ndio mana kuna kiti kinaitwa rebase kwenye uchumi ili kupandisha gdp.

Km nchi inazalisha vizuri lkn kuna import kubwa kuliko export inaweza kuathiri growth rate ya GDP
 
Katika hoja yangu kwenye posti #14, naiona shaka yako kuhusu uhusiano kati ya mfumuko wa bei na Pato la Taifa. Wapo wachumi ambao huuangalia uhusiano wa ukuaji wa uchumi na mfumuko wa bei kwa kutumia nadharia ya quantity theory of money ambayo kimsingi inasema mfumuko wa bei hutokea pale fedha zinapoongezeka kwa kasi zaidi kuliko uzalishaji wa vitu halisi.

Katika nadharia hii ongezeko “sahihi” la ujazi wa fedha (m) linaweza kukokotolewa kama ifuatavyo: m = p + y endapo kasi ya mzunguko wa fedha (velocity of money circulation (v)) haibadiliki. Hii maana yake ni kwamba, ukuaji wa fedha (m) unapaswa kuwa sawa na mfumuko wa bei (p) jumlisha ukuaji halisi wa uchumi (y).

Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia kuwa mfumuko wa bei unaotumika katika kanuni hii siyo ule unaotokana na fahirisi ya bei ya walaji (consumer price index) bali ni ule unaotokana na fahirisi ya pato la taifa (GDP deflator). Kutokana na nadharia hii tunaweza kusema kuwa ukuaji wa uchumi ni sawa na tofauti kati ya ukuaji wa fedha na mfumuko wa bei...
Hii ime base kwenye kuonyesha uhusiano uliopo kati y gdp n price fluctuation..haina effect ya moja kwa moja kwenye gdp.
 
Duh!! Hapa pagumu sasa. Kwahiyo hapa unataka kuniambia mfumko wa bei kupanda unasababisha GDP ipande?

Samahani kwa hili.
Mimi nachokiona GDP hakuna mahesabu halisi bali wanafanya makadilio ya mauzo ya nje na miundo mbinu iliokua unafanya kazi bc
 
Bado ndugu swali langu hujalijinibu. Je, kupanda kwa kumfumuko wa bei unaongeza GDP!?
Ndugu yangu kama una hamu ya kujifunza mambo ya Gdp basi lazima nikujuze kuwa kuna aina tofauti tofauti za Gdp. Natumai sitakuchanganya lakini wacha niorodheshe category mbili za Gdp ambazo zinatumika sana na wachumi.
Ya Kwanza ni Nominal Gdp versus Purchasing power parity Gdp (ppp). Wakati tunaongea kuhusu nominal na ppp, huwa hatujali sana mambo ya mfumuko wa bei. Hapa tunajali sana exchange rate ya sarafu ya nchi fulani dhidi ya dola ya marekani. Tanzania ina Gdp ppp kubwa kushinda Kenya ilhali Kenya ina nominal Gdp kubwa kushinda Tanzania.

Category ya pili na ambayo inahusu swali lako la uhusiano wa mfumuko wa bei na ukuaji wa uchumi ni nominal Gdp vs Real Gdp. Sasa hapa tunajali sana jinsi mfumuko wa bei inavyoongeza Value ya Gdp. Real Gdp ni bei ya bidhaa na huduma iliyozalishwa nchini huku ukiondoa mfumuko wa bei. Kuondoa mfumuko wa bei kwa bei ya bidhaa kunapunguza bei ya bidhaa. Kupungua kwa bei ya bidhaa inamaanisha kuwa value ya Real Gdp pia itapungua. Kwa hivyo kama unazungumzia Real Gdp vs nominal basi ni kweli kuwa kupanda kwa mfumuko wa bei kutaongeza nominal Gdp lakini hakutaongeza Real Gdp, Real Gdp itabaki pale pale. Kwa hivyo kumalizia, fahamu kwamba siku zote real Gdp huwa ndogo kushinda nominal Gdp. Fahamu pia kuwa nchi inaweza kuwa na Gdp nominal ndogo na ikawa na Gdp ppp kubwa kwa mfano Tanzania kuwa na Gdp ppp kubwa kushinda Kenya.
 
Naona umebobea kwenye masuala haya ya uchumi. Ninashukuru sana mkuu nimepata darasa la maana.
Naomba sasa unisaidie kitu kimoja. Maana ninaona wewe ni mbobezi wa mambo ya uchumi.

Ni faida zipi za kupima GDP!?
 
Venus Star,
GDP inapatikana kwa kujumlisha thamani (kifedha) ya bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini na Wazawa ikijumlishwa na thamani (kifedha) ya bidhaa na huduma zinazolishwa na kuwasilishwa nchini na Watanzania waishio nchi za nje. Thamani (kifedha) hizo zinakokotolewa kwa kipindi cha mwaka moja.
 
Naona umebobea kwenye masuala haya ya uchumi. Ninashukuru sana mkuu nimepata darasa la maana.
Naomba sasa unisaidie kitu kimoja. Maana ninaona wewe ni mbobezi wa mambo ya uchumi.

Ni faida zipi za kupima GDP!?
Faida kubwa ya Kupima uchumi ni kujua nchi gani inafanya vizuri na nchi gani inafanya vibaya. Kumbuka uchumi pia inaweza kupungua, hio kitaalamu tunaiita "recession". Sasa hivi Marekani, Japani na Nchi nyingi za ulaya ziko ndani ya "recession" kumaanisha uchumi zao zinazidi kupungua badala ya kukua. Nchi nyingi za Afrika hazitakuwa kwenye recession kwa sababu sisi hatujafunga uchumi wetu sana kwa sababu ya Corona kama wazungu.

Sasa umuhimu wa kupanga nchi kuanzia ile ambayo ina uchumi mkubwa zaidi hadi zile ambazo zina uchumi hafifu ni kuwezesha nchi masikini kupata mikopo kwa masharti rahisi kutoka World Bank na IMF. Pia nchi masikini huwa zinasamehewa madeni haraka sana, sio kama middle income country kama Kenya ambayo kamwe haiwezi kusamehewa deni bila adhabu kali. Umuhimu mwingine ni kuwezesha nchi tajiri kushikana pamoja na kutengeneza vyama tofauti tofauti vya nchi tajiri.

Kwa mfano Paris club ambayo ni nchi tajiri ambazo zilishikana pamoja kusamehe deni za nchi masikini ikiwemo za Afrika. Kuna OECD ambayo ni club za nchi zilizoendelea na zimekubaliwa kutoa loans na misaada kwa nchi masikini. South Korea ilijiunga na OECD miaka michache iliyopita kwa sababu wana uchumi mkubwa sana na sasa wao wanajiita donor country. Kuna G7 ambayo ni club ya nchi saba nzito kabisa kijeshi na kiuchumi.

Kuna G20 ambayo ni club ya nchi nzito ishirini kijeshi na kiuchumi. Afrika kusini ndio nchi pekee ya kiafrika ambao wako ndani ya G20. Kuna BRICS ambayo ni nchi tano ambazo ni nzito kiuchumi na kijeshi ila sio first world. Huwezi kujiunga na hizi clubs kama hatujui uchumi wako unatoshana vipi na kama uchumi huo umefikisha viwango.

Pia size ya uchumi inafanya World bank na IMF kurank kila nchi kuwa either developed, middle-income au least developed. Least developed hawaruhusiwi kuchukua Eurobond na madeni mengine kwa sababu least developed huwa wana matatizo ya kulipa. Lakini siku hizi least developed countries wameanza kupewa Eurobond ila kwa bei ya juu (high interest rate). Lakini middle income inapata Eurobond au loan from international banks kwa bei nafuu kwa sababu middle income ni ngumu ishindwe kulipa deni kwa hivyo inapewa haraka sana bila maswali mengi. Sasa developed countries wanapata mikopo kwa bei ya chini zaidi kwa sababu wao kamwe hawawezi kushindwa kulipa.

Badala ya kujaza server, wacha nimalize kwa kusema sababu nyingine kuu kwa nchi zote kutaka kuwa na Gdp kubwa ni kwa sababu Gdp kubwa inavutia investors kama vile nzi wanavutiwa na harufu ya choo. Wote wanajazana humo ndani. Siku zote investors watamiminika katika nchi inayo uchumi mkubwa, barabara nzuri, sheria inayofuatwa na kuheshimiwa, wananchi waliosomea fani mbali mbali. Kuna sababu nyingi za kucalculate Gdp siwezi maliza zote.
 
Mfumuko wa Bei (Inflation) ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma mbalimbali, zinazotumiwa na sampuli wakilishi ya kaya binafsi katika nchi, zinazokusanywa kila mwezi katika kila mkoa. Sasa ukifuatilia kwa Tanzania utagundua kwa miaka miwili mfululizo haukupanda bali ulishuka, kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini Tanzania (NBS)...

Kwa mfano, NBS wamefafanua kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi April,2020 umepungua hadi 3.3 % kutoka 3.4% kwa mwaka ulioishia Machi 2020...

Bishop Hiluka wa Peramiho, mfumuko wa bei (inflation) ni kipimo kinachotumika kuonesha nguvu ya sarafu ya kununua bidhaa na huduma katika nchi fulani. Kwa kiingereza wanaitwa purchasing power.
 
Bishop Hiluka wa Peramiho, mfumuko wa bei (inflation) ni kipimo kinachotumika kuonesha nguvu ya sarafu ya kununua bidhaa na huduma katika nchi fulani. Kwa kiingereza wanaitwa purchasing power.
Sawa ndugu. Hebu tunaomba udadavue uhusiano wake na GDP.
 
Back
Top Bottom