Naomba wazo la biashara, nategemea kupata Tzs 4,000,000/= (Milioni nne)

Faida n hadi mwisho wa mwezi sio hapo hapo unapomaliza mzigo
 
Nunua boda boda itapendeza kama utaendesha mwenyewe
Amini nakwambia itakusongeza
Weka mikakat, kusanya hesabu kama vile unampelekea boss
Chomoa kiasi kidogo kwa matumiz kingine save
Shida kama ni muajiriwa
 
Fanya biashara ya kuuza vyakula vya kuku vile vya asili vitakulipa mkuu.

Fanya biashara ya kuuza mahindi au unga dona sehemu za mabwawa Kama mtera au maziwa kwa wavuvi kwenye makambi itakulipa mkuu.

Fanya biashara ya kuuza nguo special za bei nafuu maeneo ya migodin itakulipa mkuu.

Fanya biashara ya kuuza dagaa wa kukaanga unapeleka mikoani au vijijin itakulipa.

Fuatilia ukisikia Kuna mgod mpya wa wachimbaji wadogo wahi ununue generator ya kufua umeme ya bei ya chini. Ukiwafungia wenye vibanda na mama lishe taa 500 kula siku unachaji 500 kila taa mwenye taa 4 buku 2000, itakulipa.

Kwa leo naishia apa. Mawazo ni mengi tutaendelea Tena.
 
Tumia pesa ikuzoee, kila mtu akifanya biashara nani ata mtuma mwenzake?
 
Kiukweli ni biashara ambayo naipenda na kila nikifikiria naona inanijia kichwani, sina ujuzi nayo mkuu🤔
Hapa inabidi kumpata mjuzi na mwenye uzoefu kabisa... anakupa ABC... mwanzo mwisho
Kuanzia vifaa, mahitaji, upikaji , changamoto hadi faida.

Ukipata taarifa zakutosha itasaidi kuoka mtaji unaotarajia kuwekeza, usipukutike bali kuongeza faida ...

Maana naona kufanya tu kwa taarifa za juu juu au vile tu akili inavyokutuma..hapo itabidi kuwa tayari kugharamika kwa hasara na changamoto zozote mbeleni.
 
Ml 4 inakutosha kabisa kununua pikipiki used 4, daily unaingiza 28k halafu zidisha Mara mwezi Mara mwaka.
Mkuu kuwekeza 4mil kupata Tshs.28,000/siku naona kama ni ndogo? Gharama ya service kwa kila pikipiki ukiondoa utabakia na kiasi gani?

28,000/day × 30(mwezi) = 840,000

840,000 x 6month = 5,040,000
Baada ya miezi sita atatengeneza hi 5mil
Ndio atapata faida ya 1mil pamoja nakurudisha mtaji huku pikipiki zikiwa salama...🤔?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…