Naombeni CV ya Miss Tanzania 2016

TAARIFA KWA UMMA

Napenda kuujulisha Umma yafuatayo;

1. Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji jana jijini Mwanza, anaitwa Diana Edward Loy na siyo Diana Lukumai kama inavyotajwa mitandaoni.

2. Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha Day na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni kwa malengo ovu.

3. Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya Chuo Kikuu chochote Tanzania au duniani bali anatarajia kujiunga mwaka huu katika chuo cha IFM kusomea masula ya kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa kulingana na ratiba zake na majukumu yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world mapya huenda akaahirisha mwaka wake wa masomo.

4. Tunawasihi watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii na si kufanya "Character assassination" lakini pia tunaheshimu haki yao ya msingi ya kuhoji masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu ambaye ni Public figure na ataliwakilisha taifa katika anga za kimataifa.

Tumuunge mkono mlimbwende wetu ili atuletee Taji la Dunia.

Ahsanteni.

Charles William
Kaimu Ofisa Habari wake.
0716719589 (wilflow101@gmail.com).

CnP
 
Unajua Elimu sio kila kitu, uenda kawa yeye kwasababu ni yeye.

Elimu yetu ya bongo ina mambo mengi yasio zingatia vipaji..!

Dunia ya sasa inaongozwa na vipaji, sasa Elimu yetu haihusudu vipaji.

Hivyo wenye kujielewa ni wale wanao wahi kuona fulsa na kuifanya kama msingi kamili wa kujingizia kipato. Kisha ndio ndio ujiendeleza kama Diamond na wengine wengi.

Watu wote walio kaa kwenye Elimu mpaka phd wanekuwa watumwa, ila walio wahi kuona fulsa, harafu wakajiendeleza kwa Elimu watu hao wanauwezo mkubwa sana na ndio waajili wenye vitu mbali mbali Nchini.

Msimkatishe tamaa binti wa watu, kila mtu atoe mawazo yake ili kumjenga zaidi ili afikie ndoto zake.

Kama vile kumsapoti katika kila jambo, ila lisiwe la kudhalilisha Taifa tu.

Bila ya kuungana na kusapotia katika mambo mbalimbali tutafeli zaidi ya hayo matokeo.
 
Alafu na wewe Mgirik nahisi hujielewi wenzio wanajadili hoja, unaandika vitu havina mbele wala nyuma au na wewe sifa zako zinalingana na Miss TZ? Au swala linalokuhusu wewe ni lipi au hadi mtu akutie kidole Kwenye macho? Hii inaitwa miss TZ nasi ni watanzania yatupasa kuyajadili Haya
 
Asante kwa taarifa kiongozi. So who came up with Lukumay and degree stuffs? Natamani ajulikane na kuchukuliwa sheria for character assassination mara moja
 
Duh hii kali aise..... Hizi figisu figisu zitaisha lini.... Waifungie maisha kabisa hii miss Tanzania maana sasa zimekua ni mashindano yakutangaza uongo
 
Hayo ya umri mtajua wenyewe. Dada miss mie naomba unipe ajira nikuendeshee hiyo ist toka Mwanza Hadi Dar..Bei yangu ni nafuu kidg
 
Asante kwa taarifa
 
Wabongo kwa kushupalia mada za kijinga najua yatafuata mabandiko ya hati yake ya kusafiri, cheti cha kuzaliwa, ushuhuda kutoka chuo anachodaiwa kusomea shahada nk.

Kila la kheri Wabongo wenzangu.
 
Kweli sikujua kama Kuna miss Tanzania na pia ningependa kujua hii issue ya degree katika mashindano yaliyopita mshiriki anapojieleza huwa hutaja kama moja ya taarifa yake kielimu,je alisema yeye elimu yake ni kidato cha nne? Maana huwezi sema elimu yako ni cheti wakati hata darasani hujakaa.
Naamini kwa shule aliyosoma humu ndani ya jamvi kutakuwa na watu wenye kumfahamu huyu binti kwa wadogo zao kusoma nae au kua jirani nae,mwisho washkaji WA A town tunaomba mtuondolee ukakasi kwa kutuletea ukweli WA mwakilishi WA nchi yetu katika ulimbwende.
 
Haya mashindano mimi naona yametushinda ni bora kuyataifisha kwa nchi jirani mfano Kenya au Uganda
 
Degree na umiss WAP na WAP kwani waso na degree hawawezi kushiriki mashindano
Wanachohoji ni kwamba hiyo degree alihitimu mwaka gani? Na kwanini wamesema ana shahada hali ya kuwa matokeo yanakataa ya kidato cha nne.kama angepitia ngazi ya cheti basi angekuwa bado hajahitimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…