Kama ya umeme kwa hiyo bei unayosema nadhani ni hizi Linkall Electrical scooter. Kuna dogo anayo.
Faida:
Umeme bei ndogo kuliko mafuta.
Haiitaji registration wala bima wala leseni.
Rahisi kujifunza sana.
Hasara:
Nina mashaka na ubora wa battery.
Range ya kilometa 60 ndogo sana.
Build quality sio nzuri sana kwani nimeona plastic zimeanza kubanduka banduka, unavoendesha kanalialia.
Haka kama unamisele mifupi ya Posta tu au Kariakoo tu, ndio kanafaa. Ila kama unapiga zaidi ya kilometa 10+ kwenda tu kazini au misele so na kurudi 20+ sidhani kama ni wazo zuri. Pia kama unatumia sana highway ni risk.
Overall Bora izi za Petrol.