Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,153
- 3,800
Kuvaa nguo zisizo za heshima ni moja ya sifa za wanamuziki wetu. Wote tumeona na tunaangalia TV chanel zetu za ndani. Siyo vyema kusimulia zaidi kinachoonekana kwenye miili ya wanamuziki hao ambacho kimaadili hasa ya Kitanzania, hakikupaswa.
Tuje kwenye mada. Ninaomba kuelezwa na mtu yeyote kama uvaaji tunaouona kwa baadhi ya wanamuziki wetu kwenye mikutano ya Rais., Vyama ni wa kimaadili na unafaa. Pia, kama haufai, ni nini kifanyike, na je ni lazima tuwe na watu wa aina hiyo kwenye mikutano yetu kama ile ya kiserikali au Kitaifa?