Naombeni kujua kuhusu sheria ya matumizi ya VPN Tanzania

Naombeni kujua kuhusu sheria ya matumizi ya VPN Tanzania

Nimehamisha mada kivipi wakati unalazimisha serekali itangaze kwenye gazeti la serekali wakati tupo katika serekali ya kidikteta isiyofuata mifumo ya kisheria!Uchaguzi huru na haki upi?

Kutumia jeshi kusimamia uchaguzi,kutumia maofisa usalama kusimamia uchaguzi,kuzima mitandao ya kijamii na internet,kuiba kura mchana kweupe,kuua wananchi tena kwa kutumia majeshi ya kukodi(huko Zanzibar),kupiga na kuweka wapinzani ndani,kupiga na kuweka mawakala wa vyama vya upinzani ndani,kufukuza mawakala wa vyama vya upinzani wakati wa kuhesabu kura,wagombea wa CCM kushinda kura nyingi kuliko watu waliojiandikisha kwenye vituo,kutishia kuua upinzani waziwazi,e.t.c,je hizi siyo sifa za udikteta?Unataka kutulazimisha tuseme kuwa hizi ni sifa za nchi ya kidemokrasia?
Uko sawa kabisa
 
Watu Tunaserereka Bila UFO VPN Basic
Wamebana Wameachia
 
Membe, bonnah, polepole jana wamepost twitter na wakati mitandao yote iko jammed, kama ni kosa kutumia VPN basi watueleze wamewezaje ku access hizo sites
Na si hao tu msemaji wa serekali amepost rais wa zanzibar amepost na wengi kweli kweli
 
Yaani hujaona sehemu waliyosema kuwa kufungua kwa namna yoyote ile mawasiliano yaliyofungwa ni kosa?
Kufunga mitandaoni bila kutoa taarifa kwa mteja ni kosa pia, ukiunga kifurushi wanakata pesa na kukupa data. Wangezuia kabisa kujiunga na internet ili kuepusha wizi wanaofanya
 
Back
Top Bottom