Nimehamisha mada kivipi wakati unalazimisha serekali itangaze kwenye gazeti la serekali wakati tupo katika serekali ya kidikteta isiyofuata mifumo ya kisheria!Uchaguzi huru na haki upi?
Kutumia jeshi kusimamia uchaguzi,kutumia maofisa usalama kusimamia uchaguzi,kuzima mitandao ya kijamii na internet,kuiba kura mchana kweupe,kuua wananchi tena kwa kutumia majeshi ya kukodi(huko Zanzibar),kupiga na kuweka wapinzani ndani,kupiga na kuweka mawakala wa vyama vya upinzani ndani,kufukuza mawakala wa vyama vya upinzani wakati wa kuhesabu kura,wagombea wa CCM kushinda kura nyingi kuliko watu waliojiandikisha kwenye vituo,kutishia kuua upinzani waziwazi,e.t.c,je hizi siyo sifa za udikteta?Unataka kutulazimisha tuseme kuwa hizi ni sifa za nchi ya kidemokrasia?