Pre GE2025 Naombeni kujulishwa kifungu kinachomruhusu Rais Samia kugombea Urais 2025

Pre GE2025 Naombeni kujulishwa kifungu kinachomruhusu Rais Samia kugombea Urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
HILI NALO MKALITAZAME.

Nawaagiza akina Kasimu na Kabudi mwende mkapekue pekue kwenye katiba yetu muone kama mama yenu nitagombea tena urais.

Hata mimi mama yenu sijui kama katiba yetu inaniruhusu kugombea tena au la, kwahiyo nawaagiza mwende MKALITAZAME kwa makini.

Na suala JENGINE, hakikisheni tunawabinya wapinzani ndani na nje ya chama kabla hawajafurukuta na kuanza kuleta "vijichoko choko".

Nimewaagiza kwa sababu nawaamini. Kabudi umekuwa kwenye Tume ya makinikia kwa muda mrefu kwahiyo nina imani na uzoefu wako. Mdogo wangu kamanda siro na wewe pia tunakutegemea kwenye "ulinzi shirikishi".

Tanzania ni yetu sote, sio yangu samia peke yangu. Tanzania oyeee!! Tanzania safiii!!

HAKIKISHENI MAMA YENU NASHINDA KWA KISHINDO CHA TEMBO.

MKINIKUNA NITAWAKUNA.

Cc: Lamomy Poor Brain mshamba_mwingine Extrovert NAMBA MOJA AJAYE NCHINI DR Mambo Jambo min -me
Daaah umefanikiwa kumfahu vizuri bi Kizimkazi
 
Wewe lete kifungu kinachosema asigombee 2025
Yeye km mgombea mwenza ukomo wa kipindi chao ni miaka 10 hakuna pameandikwa kwenye katiba mgombea mwenza anaweza kugombea urais baada ya miaka 10 ya uongozi wao.
 
Umesoma katiba lakini? Samia anaruhusiwa na Katiba na hii ndiyo mara yake ya mwisho, 2030 hataruhusiwa!
Hii itakuwa awamu ya kwanza. 2030 itakuwa ya pili. Huyo mnaye hadi 2035🤣🤣
 
Hii itakuwa awamu ya kwanza. 2030 itakuwa ya pili. Huyo mnaye hadi 2035🤣🤣
Haihesabiwi hivyo mkuu. Samia alianza zaidi ya miaka mitatu hivyo hiyo inahesabika ni awamu tosha kabisa. Kwa hiyo anaishia awamu ya 2025-2030!
 
Haihesabiwi hivyo mkuu. Samia alianza zaidi ya miaka mitatu hivyo hiyo inahesabika ni awamu tosha kabisa. Kwa hiyo anaishia awamu ya 2025-2030!
Hiyo miaka mitatu aliyoanza hakuwa amechaguliwa kwa kura kuwa rais wa JMT
 
Kaka we jua anagombea tena form ni MOJA tu CCM, mambo ya vifungu tena?
 
Iko Hivi; ni kweli Katiba yetu inaruhusu makamu wa Rais kurithi kiti cha Urais pindi Rais aliyeko madarakani anapofariki.

Swali langu, kama Magufuli angekuwepo huu ndiyo ulikuwa muhula wake wa mwisho, ina maana hata lift aliyoipata Samia ndiyo inaishia hapo.

Sasa hiki kipengele cha kumruhusu Samia kugombea tena muhula mwingine kakitoa wapi?
Kila Mtanzania ana haki ya kugombea uRais wa Tanzania kupitia chama chake. Usihangaike na Samia, nenda kwenye chama chako kachukue fomu mupambane
 
Uko sahihi ila katiba inasema urais ni vipindi viwili vya
downloadfile-1.png
miaka mitano jumla kumi, Bimkubwa akimaliza 2030 miaka kumi haitakuwa imetimia, hapo ndo kuna utata kikatiba japo kiuhalisia inatakiwa Bimkubwa aongezewe muda aliyotumikia Rais Magu ikifika 2030 ili atimize miaka kumi yake.
 
Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37 (5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.
Na wewe usidanganye watu inayosema kipindi cha kushika madaraka siyo ibara ya 37(5) bali ni Ibara ya 40(5).

Mkuu Manjagata , ni Ibara ya 40 (4), not 40 (5).

Hiyo Ibara ya 40 (5) ulioitaja haipo anywhere kwenye Katiba!

By the way, hapo La Roche hajadanganya. Yuko sahihi, nadhani tu hukumuelewa vyema. Alikuwa anaelezea Ibara ya 40 (4) kuhusu 'haki ya kugombea tena na kuchaguliwa' kwa Rais aliyerithi urais via Ibara ya 37 (5).

-Kaveli-
 
Iko Hivi; ni kweli Katiba yetu inaruhusu makamu wa Rais kurithi kiti cha Urais pindi Rais aliyeko madarakani anapofariki.

Swali langu, kama Magufuli angekuwepo huu ndiyo ulikuwa muhula wake wa mwisho, ina maana hata lift aliyoipata Samia ndiyo inaishia hapo.

Sasa hiki kipengele cha kumruhusu Samia kugombea tena muhula mwingine kakitoa wapi?
Good morning, (Habari za asubuhi)
 
Back
Top Bottom