Pre GE2025 Naombeni kujulishwa kifungu kinachomruhusu Rais Samia kugombea Urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Daaah umefanikiwa kumfahu vizuri bi Kizimkazi
 
Wewe lete kifungu kinachosema asigombee 2025
Yeye km mgombea mwenza ukomo wa kipindi chao ni miaka 10 hakuna pameandikwa kwenye katiba mgombea mwenza anaweza kugombea urais baada ya miaka 10 ya uongozi wao.
 
Umesoma katiba lakini? Samia anaruhusiwa na Katiba na hii ndiyo mara yake ya mwisho, 2030 hataruhusiwa!
Hii itakuwa awamu ya kwanza. 2030 itakuwa ya pili. Huyo mnaye hadi 2035🤣🤣
 
Hii itakuwa awamu ya kwanza. 2030 itakuwa ya pili. Huyo mnaye hadi 2035🤣🤣
Haihesabiwi hivyo mkuu. Samia alianza zaidi ya miaka mitatu hivyo hiyo inahesabika ni awamu tosha kabisa. Kwa hiyo anaishia awamu ya 2025-2030!
 
Haihesabiwi hivyo mkuu. Samia alianza zaidi ya miaka mitatu hivyo hiyo inahesabika ni awamu tosha kabisa. Kwa hiyo anaishia awamu ya 2025-2030!
Hiyo miaka mitatu aliyoanza hakuwa amechaguliwa kwa kura kuwa rais wa JMT
 
Kaka we jua anagombea tena form ni MOJA tu CCM, mambo ya vifungu tena?
 
Kila Mtanzania ana haki ya kugombea uRais wa Tanzania kupitia chama chake. Usihangaike na Samia, nenda kwenye chama chako kachukue fomu mupambane
 
 
Na wewe usidanganye watu inayosema kipindi cha kushika madaraka siyo ibara ya 37(5) bali ni Ibara ya 40(5).

Mkuu Manjagata , ni Ibara ya 40 (4), not 40 (5).

Hiyo Ibara ya 40 (5) ulioitaja haipo anywhere kwenye Katiba!

By the way, hapo La Roche hajadanganya. Yuko sahihi, nadhani tu hukumuelewa vyema. Alikuwa anaelezea Ibara ya 40 (4) kuhusu 'haki ya kugombea tena na kuchaguliwa' kwa Rais aliyerithi urais via Ibara ya 37 (5).

-Kaveli-
 
Good morning, (Habari za asubuhi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…