Naombeni Mawazo kuhusu kusoma LLM Online Uingereza ama nchi nyingine za magharibi

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
8,586
Reaction score
11,227
images (1).png
Wakuu, Ninaombeni maelekezo kuhusu kufanya masters online kwa vyuo vya ulaya na marekani, Ni njia gani rahisi ya kufanya hivyo? Naomba msaada kwa mtu mwenye uzoefu na hayo mambo.

Ni chuo gani kilicho Bora na Cha uhakika?

Mafunzo yanapatikana kwa muda gani?

Ni majira gani ya kufanya application?

Vigezo vipi vinaluhusu kujiunga na hicho chuo?

Website gani za usaidizi nizitembelee kwa maelezo zaidi?

Kwa pamoja tutavaa joho ahsanteni wakuu.

images (35).jpeg
 
Kamwene...

Kwa nini unataka kusomea Masters in Law?
 
Nina bachelor degree mkuu

Ya fani gani? Kama ni ya sheria, ushasoma na kuhitimu Law School na hivyo kusajiliwa kama wakili msomi?

Kama bado: Achana na Masters. Nenda TLS kasome usajiliwe.

Kama tayari: Kitu gani utakachosoma Masters ya sheria utakachojiongeza nacho ambacho hutakipata usipoenda kukisoma?
 
Masters Degree itaniwezesha kujoin PHD ambapo nitatumia nafasi hiyo kusoma na Law school,
 
Infact nipo job na karibu namalizia degree nataman nitakapoomba ruhusa ya masomo iwe ya miaka mingi sio mmoja tuu wa law school
 
phd bila masters

Mbona ya kawaida tu.
Vyuo vingi vya nje vinapokea wanafunzi wa PhD watokeao BSc.

Usijilimit kwa mawazo ya kizamani kwamba PhD ni mpaka uwe na Masters; au Masters ni mpaka uwe na bachelor's degrees.
 
huo utaratibu mpaka nje Labda ... na masters bila BSc asee nieleweshe kidogo
 
Ya fani gani? Kama ni ya sheria, ushasoma na kuhitimu Law School na hivyo kusajiliwa kama wakili msomi?

Kama bado: Achana na Masters. Nenda TLS kasome usajiliwe.

Kama tayari: Kitu gani utakachosoma Masters ya sheria utakachojiongeza nacho ambacho hutakipata usipoenda kukisoma?
Mshahara mkubwa ndio unatafutwa na sifa ya uteuzi.
Afrika ndio maana unaweza ukamkuta Medical Assistant ni mzuri kwenye kazi kuliko Medical Dokta kwa sababu watu wanasomea mishahara mikubwa na sio ujuzi.
 
Back
Top Bottom