naombeni mawazo yenu

Yeah ...The Dii Part.....something more? Do I need Microscope?



Rev umenifurahisha saana angles of my smile zimevuka beyond... for that asante..
Hamna mahusiano kabisaa, labda ungekua na wasi na kijana mwingine labda ungekua
umepatia, ila i keep the name no need of changing... hata hivyo Steve Dii namkubali
na tunakutana saana jamvini... bless him and you of coz..
 
Naona shosti wako awapotezee wote mana wanataka kumfanyia gwaride..
Ni hivii kaka B kaamua kukaa pembeni kumwachia kaka A..Kaka A nae ataendeleza mbwembwe zake na kumpata shosti wako halafu akivunja amri nae atamuacha..kwa huzuni itatotea siku shosti wako atamwelezea kaka B ambae atajifanya anamfariji halafu anampata na kumchezea shosti wako tena pia kumuacha kwenye mataa.
Halafu hao makaka A+B kwa kuwa ni marafiki,ushkaji wao utaendelea japo wamepitia shosti wako na kupata walichotaka..halafu hawana muda nae tenaa!..kifupi wanamtumia!!.
Mwambie shosti awapotezee au kuwa mwangalifu!!.
 


OOhhh nami ninafurahi kwa niaba yako! Meno yangu 29 yote walau yameonekana

Glorious!
 



wakati mwingine ukiangalia hili at another side of the coin,
kiukweli unaweza kuta hawa wakaka, sijui A , B hawana matatizo kabisa,
Tatizo liko kwa huyo shosti,
Cheusi hebu mwambie shosti aache hako katabia kaumalaya tafadhali,
asifikiri sifa,atambue kuwa NYUKI HAPIGWI BUSU...
 


Nashukuru dear for the vote of confidence....lol

Enways pamoja na madhaifu ya A tukumbuke kua ndo alikutanisha na was the friend before hata B, Shosti inabidi achukulie adv hio kwa kua huru na kuongea nae kuhusu feelings zake juu ya B (na akitaka isiwe awkward it is beta ajifanye haja notice the interest in her...), La muhimu kabla hajafanya hivyo inabidi ahakikishe B ana mpango dhabiti, maana haya mambo ya love hutufanya tuwe clouded in judgement na kutaka kuamini want we want... Jinsi gani atamface B hapo ni shida kidogo asianze yeye kutamka (atumie techniques zetu za kidada... kumuweka jamaa in a position wea he admits...)
 

bacha ni nin kimefanya udhani huyu dada ana katabia ka umalaya?
siwezi kumlia yamin lkn namfahamu ni dada aliyetulia kabisa na hata kaka yangu akisema anamuoa nitapokea habar kwa moyo mweupe sbb ni dada anayejiheshimu.
sio ajabu kwa mdada kuwa na hisia za kimapenzi kwa rafiki wa rafik yake.
ningependa kujua kilichokupa hisia kuwa shosti wangu ni malaya
 

Kwa nini unasema huyo shostito hana feelings na kaka A? au kwa sababu kamuona kaka B?
Mapenzi we acha tu yaitwe mapenzi. Umeona mjini unakuta kajamaa kachafu chafu alafu kabayaaaa alafu akanamashimo 10 Mererani huku mitaani kana viota 5 mambo safi kuhusu fweza angalia sasa hapo mabinti warembo wanavyo jilesi kwake.
Naamini hata kaka A angetumia mapema sanaa ya kutongoza ambapo unahamisha feelings za mwanamke ziendane na matakwa ya mwanaume basi angekuwa katika himaya ya kaka A sasa hivi.
 

fidel unaweza kuwa sahihi,lkn mm nasema alichonileza shosti na pia jinsi ninavyomfahamu,shosti wangu ndiye kasema hana feelings na kaka A.
lkn si ni rahisi tu kuelewa mtu anaposema kuwa hana feelings na mtu fulani,maana hakuna binadamu anayeweza kuwa na feelings na kila mtu.'
ngojea nijitolee mfano mm,mm kama sina feelings na wewe hata ufanye nin sitakua na hizo feelings,hata ukinipa fahari yote ya dunia,kama nitakukubali haijalishi kuwa nimepata feelings za kukupenda,no,nitakua niko na ww sbb nataka mali zako.
shosti anampenda A kama rafiki,tena anadai jinsi A anavyofanya ligi anajihisi kama anamchukia fulani hivi.
 
hapo bold nahisi kama ni wewe, eeeee cheusi, tuambie ukweli bana hahahahaa
 
Hata mie simuelewi kaka A sbb eti hadi mwenzie aoneshe nia ndo na yeye aanze fujo.
mm naona kaka A anataka ligi tu lkn hana mapenzi na shosti.
MIE SIPENDI WANAUME WASIOJIAMINI, ANZA NA b HUYO NDIO KIDUME BANA
 
kwa sasa siwezimpa mtu ushauri wowote wa kijamii as mwenyewe yanaelekea kunishinda

Hahhahaaaa nimecheka hii hadi basi, yalishanishainda ila nikipata chance nawashauri wahusika ili wasipitie path niliyopita coz was a dark tunnel sometimes nakaa chini naandika matukio na kuyasoma na kuchoma moto kikaratasi ila there is always a light at the end of the tunnel
 
Well mwambie aachane nao wote coz mwisho wa cku hao jamaa wanaweza fanyiana kitu mbaya,akae nao pamoja awachome roho kwa kuwambia kuwa ana mtu na aendelee kuwa marafiki na washkaji!
 
Hilo lipo sana,ilinitokea pia mi na rafiki yangu,pale ninapojenga uhusiano yeye naye anaanzisha,mi nikiona hizo namwachia ili aeleze nia yake unakuta anakataliwa,akishaniharibia hivo namtafuta mwingine nashangaa na yeye yupo tena,ikafikia mda nikaamua kutulia nimwangalie tu yeye apate kwanza halafu mi nitamtafuta wangu,but ikawa inajirudia same ishu,na kweli kugombana na rafiki yako ni ngumu kisa mapenzi.baadaye tukaa chini tukaelezana na ninapomfuata girl flani mi namwambia kabisa kwamba naenda kutongoza so hakunisumbua tena.
cha msingi kaka B amwambie live huko rafiki yake.na ninajua hawatapigana.
 
Huyo dada namshauri awapige chini wote wawili kwa sababu ni obvious hampendi A kwa hiyo asiingie kwenye mapenzi na mtu asompenda kisa yuko available. Pili hapendwi na B. B angekuwa anampenda asingekubali maelezo alopewa na A bila kuyafanyia kazi. Angemuuliza huyo dada ili ajue ukweli kama yeye na A wana uhusiano wowote. Kwa ufupi B alitaka kumchezea ndio maana alipoona rafiki yake A yuko interested amemwachia aendelee kwa sababu yeye hajakolea kiivyo kwa mdada.

Both A and B are players. Awe makini sana.
 

hivi unamchukuliaje pale anapokuingilia kila ukianza kumfuata binti,na je anapomfuata binti unayempenda then unaamua kumuachia,ina maana mapenzi kwa yule binti yanakuwa yamekuisha au unaamua kujikaza kisabun tu.
hata mi nadhan mwenye kama B anamsimamo atachukua hatua yeyote,mm nitamshaur binti atulie kwanza aone B atachukua hatua gani.
 

hapa wala sina cha kuongeza,,,,,
 
Subira yangu ndo iloniponzaaa,ngoja ngoja naonekana zoba,dada aache kujiuma uma A aambiwe apishe barabarani asije gongwa na lori.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…