Naombeni Mchongo, Biashara au Part-time ya kupata 15k-30k kwa siku

GEMO

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2016
Posts
250
Reaction score
277
Ishu yako inategemea mambo mawili makubwa

1.Mazingira uliyopo

2.Mtaji

Mf ukinunua boda boda 2 ukawapa vijana kwa siku utapata 14,000/= boda 2 kuzinunua ni 4.8m -TVS

Ukifungua saloon 2 za kiume kwa 1.5m kwa siku utapewa 20,000/= kila saloon elfu 10.

Ukiwa na vijana watatu wa kuuza mayai...ukanunua baiskeli 2 kwa 120,000 kila moja na kuwa na mtaji wa 350,000/= sawa na trei 50 kwa siku kila trei ukapaga kiwango cha kawaida cha sh 1000 utapata elfu 50 vijana watatu posho plus msosi ni 15,000/= unabaki na 15,000/=


Ukinunua bajaj kwa 7.5m kwa siku utapata 15,000 unayoitaka

Ukinunua nisan au Costa kwa siku utapata around 40k to 50k

Swali hapo la muhimu Je una mtaji wa sh ngapi ?

Upo tayari kiasi gani kupambana
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Fanya ,,,,uwe unatembeza mtaani ...hapo wateja utapata lakin maofisin inakua ngumu.

Jaribu biashara ya viatu mtumba kwa upande wa watoto wakike lakin use unatembeza mtaa kwa mtaa.
 
life ant easy kiivo asee .hata services ya kuingiza hiyo 15k bila specified skill sio rahisi kupata
Kijitonyama wapo washakaji wawili wanaingiza ×2 ya hiyo bila skills wala Mtaji...nahuzunika mimi niliikosa tu nafasi tu.
 
life ant easy kiivo asee .hata services ya kuingiza hiyo 15k bila specified skill sio rahisi kupata
Rajabu a. K. A konde boy hapa kila siku anaondoka si chini na 16,000.
Mtaji wake ni nguvu zake za kuendesha baskeli. Kuna kipindi anapataga zari mpaka 20,000.
 
Rajabu a. K. A konde boy hapa kila siku anaondoka si chini na 16,000.
Mtaji wake ni nguvu zake za kuendesha baskeli. Kuna kipindi anapataga zari mpaka 20,000.
Mtonye mwana basi naye apate kuingiza hicho kiasi
 
Kazi ya kuchimba mabwawa ya samaki.
 
Sasa hivi corona virus mchongo umesimama.
Lakini mbona kuna post huwaga nawekaga humu natafuta vijana siwaonagi? Wengine ukiwaambia kuendesha baskeli anaingia mitini kabisaaa.
Yamkini sasa atakusikia vizuri ,wewe mpe kijana wazo
 
Nenda kwa wauza chips tafuta oda ya trei 10 kila siku.

Nenda jwa mfugaji wa kuku chukua mali kauli....mshawishi hadi akupe trei 10 kwa sh 6000 kila trei ukauze mtaani.

Hadi hapo hujatumia hata 100 ni USHAWISHI.

Kodi baiskeli kwa buku then zunguka mtaani kwasababu hujazoeleka utachukua muda kuuza ila wakishakuzoea unauza fasta tu tena wao ndo watakupa oda.Unawauzia 7000 kila trei unapata buku.

NB; INATEGEMEA UPO TAYARI KUJITOA KIASI GANI....JITOE UFAHAMU ULIOUVAA KUHUSU STATUS YAKO, HESHIMA,KUOGOPA MAWAZO YA WATU ZILE WATANIONAJE,NITACHEKWA .....VAA UHALISIA UISHI

GEMO
GEMO natafuta hela ya kula na ya tahadhari endapo nitaumwa. Sina mtaji mkubwa, nina 20,000 tu hapa tena kesho itapungua nikinunua chakula

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…