Naombeni Mchongo, Biashara au Part-time ya kupata 15k-30k kwa siku

Naombeni Mchongo, Biashara au Part-time ya kupata 15k-30k kwa siku

Sasa hivi corona virus mchongo umesimama.
Lakini mbona kuna post huwaga nawekaga humu natafuta vijana siwaonagi? Wengine ukiwaambia kuendesha baskeli anaingia mitini kabisaaa.

Ngoja nije chap Mkuu amu [emoji1545]
 
doh unatafuta mchongo wa 15K per day kwa mtaji wa 20k, brother try another figure lamda 1.5k [emoji23][emoji23][emoji23]
Bro, huelewi biashara mfano machungwa ya tanga kwa arusha moja ni 50-70 kwa jumla. Akinunua machungwa 250 ni 12,500-17,500
Fungu moja la machungwa ma5 huuzwa 1,000/=. Hivo kwa machungwa 250 atakua na fungu 50 za machungwa ambayo ni 50,000/=.
Ukitoa mtaji ambao hauzidi 17,500 anabakiwa na 32,500/=
Nimeongelea machungwa ni biashara na uzoefu nayo, na idadi hiyo ni ndogo sana kwa machinga anayeuza kwa kupanga chini pembezoni mwa barabara.
KUA NA MTAJI MKUBWA SIO KUPATA FAIDA KUBWA...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
costa wanatoa 90 , na sasa level seats wamepunguziwa elfu 10 tu ...(jana nikiwa naelekea Tandika nimepiga sana story na dereva) level seats na anapelekea 80

Sent using Jamii Forums mobile app

Basi wamiliki wa magari wanapata hasara yani ninunue gari costa Milion 35 sijui arobain plus maushuru sijui bima sijui trafic sticker na service nifanye alafu nikusanye 80 per day means kwa mwezi 2,400,000 yani 28,800,000 kwa mwaka huu ni ungese kabisa asee apo pay back period ni baada ya miaka 2 au 3


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wazee niende moja kwa moja kwenye mada. Najishughulisha na kuuza used materials, furniture, electronics nk ( kwa asilimia kubwa Im a middleman)

Lakini hizi siku mambo ngumu asee[emoji19]. Naombeni mchongo wowote, fursa, biashara yoyote nipate angalau 15k (kula na emergency)

Ni hayo tu. PM yangu iko wazi

==========
Ushahuri wangu ni kwamba, ili upate hiyo 15k na zaidi kwa muda mfupi,
1. Tambua elimu yako au ujuzi gani ulionao
2. Baada ya hapo, tafuta kujua ni changamoto gani jamii inakumbana nazo ambazo zinaweza kutatuliwa kwa elimu au ujuzi ulionao
3. Anza kutatua changamoto hizo pesa zitakuja zenyewe kwa wingi.

Ukihitaji watu wakwambie biashara ya kufanya utapewa biashara ambazo yawezekana watu wasiwe na uhitaji katika jamii yako na mwisho wa siku ukapoteza muda mwingi kwenye kitu ambacho watu hawako tayari kulipia.
 
Basi wamiliki wa magari wanapata hasara yani ninunue gari costa Milion 35 sijui arobain plus maushuru sijui bima sijui trafic sticker na service nifanye alafu nikusanye 80 per day means kwa mwezi 2,400,000 yani 28,800,000 kwa mwaka huu ni ungese kabisa asee apo pay back period ni baada ya miaka 2 au 3


Sent from my iPhone using JamiiForums
We ulitaka iwe baada ya miaka mingapi ? wastani ni miaka 2 hadi mitatu kwa biashara yeyote ile ya gari , iwe bus , iwe lorry za mizigo iwe dalala wastani ni huo huo

NB. baada ya hiyo miaka miwil, hiyo gari waweza kaa nayo hadi ukafika mahali ukasema basi inatosha hata miaka 20 mbele, sasa piga hesabu itakua imekuingizia gari ngapi ? na zenyewe zimeingiza ngapi ?

manake kama miaka 2 imerudisha pesa yake..hiyo pesa unaongeza gari , zinakua mbili.. hutotumia miaka miwil tena kuingira gari , unatumia mwaka mmoja , zikiwa tatu sio mwaka ni miez nane mpaka 10 unaongeza chombo , zikiwa nne miez 6 chombo , tano , miez 4 chombo.. within 10 years...uko mbali mno , pengine unafikiria kuachana na biashara ya dalala uagize bus kadhaa... ndivyo biashara inavyokua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ishu yako inategemea mambo mawili makubwa

1.Mazingira uliyopo

2.Mtaji

Mf ukinunua boda boda 2 ukawapa vijana kwa siku utapata 14,000/= boda 2 kuzinunua ni 4.8m -TVS

Ukifungua saloon 2 za kiume kwa 1.5m kwa siku utapewa 20,000/= kila saloon elfu 10.

Ukiwa na vijana watatu wa kuuza mayai...ukanunua baiskeli 2 kwa 120,000 kila moja na kuwa na mtaji wa 350,000/= sawa na trei 50 kwa siku kila trei ukapaga kiwango cha kawaida cha sh 1000 utapata elfu 50 vijana watatu posho plus msosi ni 15,000/= unabaki na 15,000/=


Ukinunua bajaj kwa 7.5m kwa siku utapata 15,000 unayoitaka

Ukinunua nisan au Costa kwa siku utapata around 40k to 50k

Swali hapo la muhimu Je una mtaji wa sh ngapi ?

Upo tayari kiasi gani kupambana

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimependa comment yako naomba niongezee kidogo....
Ukipata Eneo zuri lenye vjana wengi hasa wanachuo (Malimbe au Mkolani au Bwiru karibu na chuo cha Mipango ) ukawa na ;
1- Tv 2 inch 24 @300k =600k/=
2- PS-3 2 @ 360k@=720k/=
3-Chumba kwa Bwiru unaeza pata cha 40k per month
Jitahidi uweke games nzuri kama PES 2019/2020,FIFA 19,GTA V
Hapo 15 mpaka 20k per day ni uhakika
I've been doing this kwa muda sasa so nna Experience kidogo
 
Endelea na udalali usikate tamaa kuwa mjanja ingia Makumbusho kajimix na wauza simu pale. Dalali Makumbusho wa simu tu wa kawaida hakosi 50k kwa siku bila mtaji wowote. Mtaji wako ni hio smartphone yako.


Sent using Jamii Forums mobile app
Nina ushuhuda kwa hili
Niliweza kuishi kwa zaidi ya mwaka kwa kazi hii, yaani ilikuwaga sim na Mimi Mimi na sim,
Miamala ya tigo pesa ilikuwa inaingia tu, mpaka nilipopata mtaji nikasepa
 
Nina ushuhuda kwa hili
Niliweza kuishi kwa zaidi ya mwaka kwa kazi hii, yaani ilikuwaga sim na Mimi Mimi na sim,
Miamala ya tigo pesa ilikuwa inaingia tu, mpaka nilipopata mtaji nikasepa

Acha tu vijana hatujui tena saiv kupata wateja wa bidhaa ni rahisi mno na hii mitandao yetu. Bidhaa zipo nyingi mno kuna magari, tv, simu, nyumba za kupanga, nguo, etcetcetc yaani udalali una hela balaa wewe kuwa mjanja tu hukosi 50k kwa siku
 
Back
Top Bottom