Naombeni Mchongo, Biashara au Part-time ya kupata 15k-30k kwa siku

Ukitaka kujua utamu wa ngoma ingia uicheze.
 
Wanachuo si wana game zao kwenye PC na katika wanachuo watatu mmoja ana PC na hiyo moja wanatumia room yake na jirani.
Anyway ilikua biashara yng ya utotoni. Hizo 10k-15k nilikua nazikusanya sana plus jioni ikifika naikodisha kwa 5k asubui imerudishwa naendelea na biashara. Nilikua natumia PS2.
 
Tatizo connection

Tatizo connection kivipi? Hakuna boss atakayekukatalia kumletea wateja huyo boss hayupo duniani apa nenda kkoo au makumbusho kajuchanganye na wenye mali waambie unapost bidhaa zao unaleta wateja uone kama watakukatalia tengeneza brand yako vizuri uone kama hukosi ata laki kwa siku kuna washkaji makumbusho vijana tu wana piga hela ndefu kupitia mitandao ya kijamii.
Tatizo hii mitandao vijana wengi tunatumia kusoma udaku na kufatilia mademu ila kuna wengine wanakuwa matajiri kupitia hiihii mitandao.
 
Nimekupata mkuu
 
Acha tu vijana hatujui tena saiv kupata wateja wa bidhaa ni rahisi mno na hii mitandao yetu. Bidhaa zipo nyingi mno kuna magari, tv, simu, nyumba za kupanga, nguo, etcetcetc yaani udalali una hela balaa wewe kuwa mjanja tu hukosi 50k kwa siku
Mtaji bando la wiki, smartphone yenye uwezo mkubwa wa utunzaji chaji, na nauli 2000 yakukufikisha mjini endapo deal Ni kubwa kuogopa wenzako kukupiga ganji

Ma group yakutosha
Fb,insta, WhatsApp, telegram

Na ujue hasa kuchat
 
Ni kweli kabisa mkuu....Lakini ile hali ya game kua displayed kwenye screen kubwa huleta hamasa na ka upinzani flani
 
Biashara ya betting imerud,unatakiwa kuwa na smartphone ya 100,000 tu na bando la Airtel la wiki 1500/=,mtaji 40,000/= unatengeneza mikeka 4 kila mkeka unaweka stake 10,000/= kila mkeka uwe na odds kuanzia 3-4 ina maana mkeka mmoja utapata 30,000-40000 Kama utatumia kampuni ya parimatch,let say ukiwin mikeka miwili Kati ya minne utakuwa umepata jumla 60,000-80,000 kwahyo ukitoa kwenye mtaji utakuwa na faida ya 20,000-40,000
NB:Chamsingi inatakiwa uwe unajua kuangalia siku ambazo Kuna mechi kuanzia 8 na kuendelea,tembelea olbg.com,statarea.com na forebet.com
 
acha utani mkuu, kwa mtaji 20k!?
Kweli kwa huo mtaji wake. Kama hajui kupika maandazi anunue mihogo au viazi akaange. Uchawi kachumbari. Anapiga viUri tuu.. Anakata vipande hata akiuza mia mia anapata
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] Bado services
 
una zungumzia arusha?
 
samahani mkuu wewe unafanya hii biashara?
Niliwahi fanya hio biashara kama sehemu ya kuongezea kipato. ..inalipa vizuri ila changamoto za wenye mitaa yao hasa wazazi wa kale wasojua technology utakutana nazo kuzisolve vema kabisa jitahidi walau uwe na leseni ya biashara plus juana walau na askari wawil watu wa karibu na unapofanyia kazi....Nawasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…