mtoto ya simba
Member
- Jul 6, 2025
- 14
- 19
Naweza kufanya tatizo sina chaguo lingine na kazi sina lazima nipambane tuKijana kazi kama hizo zinahitaji moyo na ukihitaji kazi ya usimamizi tu hutapata kwa hapa, kazi zote zinahitaji nguvu kubwa pia pesa zake hazidumu zaid sana utaisha na kukonda bila sababu za msingi, binafsi ninauelewa mkubwa wa madini ya dhahabu nimefanya kazi za aina hiyo si chini ya miaka mitatu, kiufupi ni kazi yenye mchakato mlefu kwa mtafuna mandazi wa kudumu kama wewe wa hapa dar sidhani kama utaweza.
Sawa asante kwa ushauri wakoKaka hii kazi hakuna cha connection nenda sehemu hizi huwezi kosa japo yataka moyo.Wale majanja wanaofanya hizi kazi sijawahi waelewa hata kidogo.Nenda Mwime,Mgusu,Nyarugusu,Nyakagwe,Nyamishiga(haya maeneo yanapatika nShinyanga na Geita)
Ushauri mzuri labda nenda sehemu zenye machimbo yaliyochini ya makampuni ya kigeni(naongelea uchimbaji mkubwa) unaweza toboa labda.
Kama ni hivyo tuliza ubongo uone ni sehemu gani inakufaa, maana machimbo ni mengi nchini, nenda sehemu husika kama ni mpambanaji kweli huwezi kukosa kazi ndani ya siku mbili tu, ukweli ni kwamba kazi huko ni nyingi maana watu hukimbia wenyewe sababu ya ugumu wa kazi, au wengine huwa wanahitaji muda wa kumpumzika hivyo unaweza kutumia nafasi hiyo ya mapumziko yao kupiga kazi, kikubwa jenga nidhamu ya pesa na jiepushe na starehe vishawishi ni vingi huko.Naweza kufanya tatizo sina chaguo lingine na kazi sina lazima nipambane tu
Jiji la dar linaendelea kujengwa ni bora uwe saidia fundiHabari wa juu
Nimekuja hapa kwa lengo moja tu natafuta mtu wa kunishika mkono anayejihusisha na mambo ya madini
Mimi ni kijana wa miaka 26 nipo Dar es Salaam
Lengo la kuja hapa ni kuomba kama kuna mtu anayejihusisha na maswala ya madini anasehemu ambayo anafanya uchimbaji ambayo anahitaji vijana wa kufanya hiyo kazi mimi nipo tayari kuja kuifanya hiyo kazi kwa nguvu zangu zote.
Sijawahi kufanya hiyo kazi ila hakuna aliyeanza akiwa anajua kila alianza mwanzo wa kuelekezwa hivyo naombeni kama yupo huyo mtu wakunishika mkono na anishike sina kazi nipo nipo tu mtaani sihitaji kujihusisha na shughuli yoyote chafu.
Kama nitapata na hakika nitafanya kwa uwezo mkubwa zaidi sina cha kuwalipa ila nguvu zangu itakulipa zaidi kwani nitaifanya kwa juhudi kubwa sana.
Muwe na siku njema msaada wako ni muhimu na wa thamani sana kwangu