Kwa aina hiyo ya mkopo nenda Benki ya Wanawake Tanzania (TWB). Wao wana utaratibu wa mikopo ya vikundi. Unaweza ukapata mpaka milioni moja bila kuweka dhamana yoyote. Kinachohitajika ni wewe kujiunga katika kikundi cha watu watano watano.
Natumaini wewe na wenzio mnaweza kutumia fursa hii adimu kujikomboa kiuchumi. Tafadhali zingatia kuwa ukipewa mkopo uulipe ili wewe uweze kukua kibiashara.