Naombeni mnipe ushauri juu ya uuzaji wa karanga kutoka Dodoma

Naombeni mnipe ushauri juu ya uuzaji wa karanga kutoka Dodoma

Cyrill rogath

Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
6
Reaction score
3
Naitaji kujua karanga za dodoma zipo katika hali gani juu ya soko lake na bei zake kwa kilo moja?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Karanga zipo nyingi Tabora na kipindi hiki ndio msimu wake mpaka mwezi wa sita...nyingi wananunua wanyarwanda kwa kupitia madalali wao..
 
Kanunue karanga mkoa wa tabora hasa wilaya ya kaliua nadhani debe moja ukikoboa ile ya maganda ni kilo tano ambapo wastani sokoni ni shilingi 2200 kwa kilo moja hivo inafaida mara mbili, soko kuu la hizo karanga ni Rwanda na Uganda japo naona mwaka. Huu wanunuZi hawajaingia nchi hizo hupenda karanga nyekundu na ndio wanunuzi wakubwa kwa kanda ile.
 
Na debe moja ya maganda itakua haizidi shilingi 5000, kama hauna mtaji unaweza kununua tabora na uende kuuza Kahama. Kwa bei za pale kahama
 
Mwaka huu mazao yatakua na pesa sana hasa mpunga na maharage, maana maeneo mengi watu hawatopata mavuno ya kutosha hivo kutakua na uhaba kama unaweza kuweka stock ya hayo mazao utapiga noti kiaina huku ukisubiri uchaguzi mkuu 2020
 
Karanga ya Dodoma ni nyeupe na soko lake kubwa ni soko la ndani hua silifahamu vizuri, lakini wale kampuni ya smart wanaotengeneza diamond karanga naona walikua wananunua sana sijui kwa sasa kama wanauhitaji au lah unaweza kuwatafuta muhojiane zaidi
 
Asee hakuna mwaka maharage mengi kama mwaka huu hauna data kamili mkuu
Chimba uende mpaka vijijini utanambia acha kutabili kama shekh yahaya
Mwaka huu mazao yatakua na pesa sana hasa mpunga na maharage, maana maeneo mengi watu hawatopata mavuno ya kutosha hivo kutakua na uhaba kama unaweza kuweka stock ya hayo mazao utapiga noti kiaina huku ukisubiri uchaguzi mkuu 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom