MAPENZI YANANITESA NIPENI USHAURI
Nimefikiria kwa muda mrefu naona nazidi kupoteza muelekeo. Naombeni ushauri wenu wa mawazo naweza kufarijika kwani nipo njia panda. Kuna kaka nilikutananae tukaanza kupendana kama unavyo jua mapenzi yanavyo anza, alinieleza kila kitu kuhusu yeye kubwa aliniambia anampenzi wake lakini wanapenda kuishi wote kigezo dini zao ni tofauti hivyo uwezekano wa kuendelea kuwa wote ni mchache mimi nili mkubalii kwani nilikuta tayari nimeshaanza kumpenda sana.
Hivi sasa mm nina mimba, na yeye ananiambia na yule mpenzi wake pia anamimba mimi sikujali. Ananilazimisha nikatoe mm sipo tayari nimemwambia sitakusumbua kwa lolote kwani mimi nina kazi yangu lakina haelewi ananitafutia mpaka watu waje wanishauri nikatoe. Naombeni ushauri nifanyaje kwani sijielewi kwani bado nampenda sana.