Naombeni mnisaidie wazo la kuongeza biashara

Hosea09

New Member
Joined
Jan 3, 2023
Posts
1
Reaction score
1
Nafurahi na napendezwa sana kuwa kuwa ndani ya jukwaa hili

Binafsi nafanya kazi ya kusajili laini za mitandao yote, kurudisha line zilizopotea na kutatua matatizo mbalimbaki ya simu za wateja kujipatia kipato.
Nimefanya kazi hii almost miaka 03 sasa nipo Chato mkoani Geita japo mzunguko sio mkubwa sana ila namshukuru Mungu kwa kibali alichonipa cha kuaminiwa na wateja wangu

Lengo la kuja hapa naomba mnisaidie mawazo ya kupanua biashara yangu niongezee biashara gani yenye mzunguko na faida nzuri ofisn kwangu, nina gazebo kubwa natamani niongezee biashara nyingine nina mtaji wa laki 05.
Naombeni mawazo yenu wakuu.
 
Vifaa vidogodogo vya electronics na simu kama testa, chaja bulb, kava, protector, batteries nakadhalika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…