Confidence! Jiamini kabisa na uoneshe kwa ishara ,usijibu maswali kama roboti hata ukiwa umekaa hakikisha mikono macho na vitu vingine vina move kwa kuonesha vitendo na ishara hasa mikono ukiwa unajieleza! Ukiganda sana utajikuta una tetemeka!
Zingatia muda! Wanamchezo wa kukwambia wana maswali kadhaa na muda wako ni dakika kadhaa! Kwa hiyo hakikisha kuwa unafanya time management kwa kujibu maswali kwa uhakika na sharp kidogo mfano swali la tell us about your self lisikuchukulie zaidi ya dakika mbili na ikiwezekana kalipange kabisa kwenye daftari in short na uliweze kulieleza ndani ya dakika mbili au tatu maana wale hawajali kama utatumia muda wote kujieleza tuu halafu watamwambia umabakiwa na maswali manne na dakika unazo kumi tuu…kwa hiyo unatakiwa time manager mkubwa hawaongezi muda ukiisha!
Answers with Examples…. Hakikisha ikiwezekana unapojibu maswali yao unaweka na mifano kabisa na unapojibu waangalie usoni bila kujali unakwenda chaka au lah elezea kwa undani usikubali kujibu juu juu kabisa usikubali!
Usithubutu kusema sijui! Hakikisha kila swali unajibu usikubali mbele ya pannel kunyanyua mikono juu kwa kusema sijui..hakikisha unapata cha kuongea usikubali kunyanyua mikono…. Hata wakiguna au kucheka wewe endelea kuchapa na kujibu maswali….
Hakikisha unajibu maswali yote na hata itategemea na jinsi unavyofanya management ya muda toka mwanzo na kutokubali kutojibu swali kisa hulijui…usikubali kuondoka hujajibu swali maana kuacha swali ni kujitoa kwenye mchezo…
Ukitoka kwenye chumba cha kukandwa usikubali kumwambia mwenzio maswali uliyoulizwa na majibu ukitoka kimbia kama mwehu vile…interview ni mchezo wa namba ..mwenye namba nyingi ndio mshindi na mkifungana unawekwa kwenye data base mwezio anapangiwa kituo haraka…ukimpa maswali maana yake yeye atajipanga na anaweza kukupiku kabisa!