Naombeni msaada jamani

salito

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2011
Posts
1,406
Reaction score
731
Jamani wana JF hivi mnalizungumziaje swala la wapendanao kuwa na dini tofauti?linamadhara gani?faida yake je?vipi kuhusu wazazi kama hawabariki swala hilo ni uamuzi gani unafaa?dini je? nisaidieni jaman maana me mwenzenu hili jambo vizuri.
 
Kwani wewe dini gani?Niambie nijaribu kukusaidia!
 
Jamani wana JF hivi mnalizungumziaje swala la wapendanao kuwa na dini tofauti?linamadhara gani?faida yake je?vipi kuhusu wazazi kama hawabariki swala hilo ni uamuzi gani unafaa?dini je? nisaidieni jaman maana me mwenzenu hili jambo vizuri.
Una maana gani?
Rudi idogo nyuma kabla ya kuja kwa dini za wazungu, je unadhani kikwazo hiki kilikuwepo?
Pia inategemeana na hatima ya hao wapendanao ninini!...kama ni pass-time haina shida, ishu huenda ikaanza kuleta complication wakati wa kuchumbiana hatimaye kuoana!
Hata hivyo haitakiwi kuleta shida iwapo wahusika wataweka sawa mambo yote kabla ya kuingia kwenye hatua hizo.
 
as long as mna mapenzi ya kweli swala la dini halitasumbua.
 
PakaJimmy dini za wazungu ni zipi hizo?
 
Dini ya kiislam inaruhusu mwanaume wa kiislam kumuoa mwanamke mkristo kwa sharti atambadili dini pia watoto wafate dini ya baba.

hairuhusiwi kwa binti wa kiislam kuolewa na dini yoyote ile except muislam , other wise binti atoke uislam na kufata dini ya mumewe!

ushauri wangu, dini si kikwazo katika penzi la kweli , kaeni chini mshauriane kwa mapenzi...........
 


Sijakuelewa kidogo,wahusika waweke sawa mambo kivipi?
 
Salito,

Swala la dini hapo mzee mh uwe makini sana coz shida inaweza kutokea kubwa iwapo mtaoana halafu mmoja atafariki kati kati ya safari
 
Salito,

Swala la dini hapo mzee mh uwe makini sana coz shida inaweza kutokea kubwa iwapo mtaoana halafu mmoja atafariki kati kati ya safari

Ndio hapo napoomba ushauri wenu wana jf,niwe makini huku nikizingatia nini?
 
Wewe kama ulivosema ni muslamu hilo jambo liko wazi kuwa huwezi kuwa na yeye labda abadili dini ndoa hahisihi watu wenye dini tafauti usifate mkumbo wa dunia fata dini yako
 
Yote inategemea na msimamo wenu wakati wa maisha yenu ya ndoa. Mwanzo mwanzo mnaweza msiwe na tatizo nyinyi wawili tu lakini matatizo yakaanza wakati mkipata watoto, kila mmoja kutaka kushinikiza watoto wafuate dini yake. Mkisema muwape watoto uhuru wa kuamua wenyewe mtakuwa hamwatendei haki katika malezi ya udogoni kwa kukosa mafunzo ya kiimani. Huwezi kumpeleka mtoto kanisani, msikitini, hekaluni...kwa wakati mmoja. Ili kuepusha hayo, ni bora mkajadiliana na kukubaliana kabla ya ndoa nini mtafanya katika malezi ya watoto wenu.
 
Kuishi pamoja kwa wenza kwa dini tofauti ni mtihani kwa watoto iwe mmeachana ama mnaishi pamoja hii kitu imevuruga sana familia yetu kwani watoto wengine hujiita mi mwislam mkristo. Nashauri kubalianeni kuwa na imani moja Mungu wetu ni yule yule ingawa njia za kufika kwake ndizo zenye tofauti.
 
ni makubaliano yenu nyie wawili mliopendana , mkikubaliana kuhusu izo iman zenu bs inatosha.
wazaz mnawaweka 2 sawa, me nadhan dini sio big deal kiivyo. kama mmependana u discus n then u conclude bs.
 
Kaeni chini mkubaliane, mwaweza tu kuoana hata mkiwa na dini tofauti.
 
Inategemea na family of origin kwenu wote (mpendanao)

Kama ni nucleus hapo its all up to you
Kama ni extended type in which mpaka mume wa shangazi naye anapewa room ya kuchangia mahusiano yenu hapo kazi ni kubwa kuliko hiyo ndoa yenyewe

So angalia familia zenu kwanza then weigh out
 
Wewe kama ulivosema ni muslamu hilo jambo liko wazi kuwa huwezi kuwa na yeye labda abadili dini ndoa hahisihi watu wenye dini tafauti usifate mkumbo wa dunia fata dini yako

ni kweli usemalo lakini moyo wa kupenda nao mhh..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…