Kutumia vitu vyenye ncha kali kama sindano wembe au visu ni hatari kwa maana vinaongeza uwezekano wa kuambukizwa virus vya ukimwi na hepatitis.
Ili kuambukizwa virus vya ukimwi na hepatitis kwa njia hii ni lazima maji maji toka kwa mgonjwa yenye virus yaungane na maji maji ya mwilini mwako kwa maana hiyo ni lazima uwe umejichubua au umejikata. Bila michubuko au vidonda virus hana uwezo wa kutoboa intact skin.
Matumizi sahihi ya ARV husaidia kupunguza kiwango cha virus mwilini lakini haviishi daima, kwa maana hiyo uwezekano wa maambukizi pia hupungua kidogo japo usidanganyike kuwa hakuna uambukizo.
Kama ni ndani ya saa 72 Nenda VCT au CTC iliyokaribu na wewe kwa uchunguzi. Maana Leo waweza singizia hicho kiwembe Kumbe tayari tangu zamani ulisha pata maambukizo. Kama Huna maambukizi utapewa PEP (post exposure prophylaxis) na kama Una maambukizi tayari utapewa ARV for life. Na kama ni baada ya 72 hrs pia Nenda endapo huna maambukizi utapewa ushauri na kupewa ratiba ya serial check up.
Pole sana