Naombeni msaada juu ya wazo langu

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
930
Reaction score
1,290
wakuu naombeni mawazo yenu hapa,

Hivi, kuna watu wana shida ya pesa ndogo ndogo ambapo siku hiyo imempiga chenga kutafuta, au kukopa, au mtu unakuta siku hiyo hali ni mbaya ya kiuchumi, ameenda job amekosa pesa ya kula, au kuna mtu mwingine mchana hali ni mbaya hajui atakula nini?

Sasa nikaona solution nianzishe kitu nitakachokiita min loan shop, kwa maana nitakuwa natoa mkopo wa kuanzia shilingi 2000-50000, na riba itakuwa ni 10%, kwa maana mtu akikopa 2000, atalipa 3000, kwa muda wa siku moja au siku mbili, hapo itategemea na kiwango unachokopa, na dhamana yake itakuwa labda unaweka simu, au kitu chochote chenye thamani ya juu ya pesa.

Kama nitaweza kupata watu 20 kwa siku, watakao kopa 2000 na kurudisha 3000, so faida inaweza kuwa 20000, lakini pia risk haitokuwa kubwa sana, maana mtu hawezi kimbia na 2000.

Naombeni mwazo yenu wadau, na wenye kuongeza au kupunguza juu ya wazo hili,

Asanteni
..
 
Wazo zuri ila hesabu zinakushinda hivyo unakuwa hueleweki vema. Unasema mtu akichukua mkopo atalipa na riba ya asilimia 10. Lakini mfano wako ndio majanga kwa sababu endapo mtu atakopa sh 2000 halafu alipe sh 3000. Riba ya sh 1000 siyo asilimia 10 kama unavyodai. bali ni asilimia 50. Kama unataka asilimia 10 kwenye sh 2000 basi atakulipa sh 2200. Nafikiri nimeleweka kama na mimi nimekosea basi nikosolewe pia.
 
asanteni, bado naendelea kupokea michango yenu.
 

Na mimi nilitoa macho hapa, hadi nikashika kikokotoo changu kuhakiki mahesabu,
 
Reactions: Kig

Kama umewaza mtu akikopa 2000 atarudisha 3000 futa kwanza hilo wazo maana hiyo sio asilimia 10, piga mahesabu vizuri halafu urudi, kama mimi nimekosea basi nijulishe mahesabu ya riba yanatafutwaje?
 


Tembo wangu hii biashara umeanza kufeli kabla hujaanza maana hesabu zinaonekana ni mama mkwe kwako hivyo unazionea haya!
 
Kweli hesabu ni janga la kitaifa yaani 10% ya 2,000 ni 1,000? Next time bwana TEMBO WANGU 10% means 10/100,kwa hiyo (10/100 ) X 2000=200,sawa? kwa hiyo kama ni 10% mkopaji anatakiwa kurudisha 2,000+200=2,200. Narudia % means anything over 100 ,right? Lesson 1 finished!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…