Naombeni msaada kwa mtu anaejua biashara hii ya kuuza jeans za kike

Golden Trust

Member
Joined
Jan 21, 2023
Posts
33
Reaction score
44
Habari wanajamii forums...
Naombeni msaada kwa mtu anaejua biashara hii ya kuuza jeans za kike au ambae anafanya au alishafanya ,nahitaji kuuza jeans ambazo sio za mtumba, yaani kufungua duka la kuuza jeans tu..Sasa naombeni ushauri ndugu zangu kwa mambo yafuatayo.
1. Mtaji wa hii biashara inaweza cost shng ngapi.
2. kwa Dar machimbo ya kupata hizo jeans ni wapi na bei yake kwa jumla
3. Changamoto zake ni zipi.
4. Bei ya midoli ni shng ngapi.

Naombeni sana msaada ndugu zangu
 
Maswali mengi lakini ngoja tusaidiane.

1. Midoli ipo ya full na ipo ya kuanzia kiunoni kushuka chini. Unaipata Kariakoo.
Ukienda kwa maduka ya jumla ina range kuanzia elfu 30 50 80 hadi 130 inatofautiana size, shape na material.

Mfano huyu anauza reja reja, na mtandaoni so unaweza guess jumla itakua ngapi.

Mwingine:



Hope utapata idea kwa jumla, let's say kuanzia 5 utauziwa kwa bei gani.
 
2. Wanawake wengi wanapenda nguo cheap, kwasababu hawana haja ya kukaa na nguo 5 years kama sisi.

Kwahiyo watataka kununua jeans za elfu 5, 7, 10, 15 nyingiii kuliko kununua ya elfu 30 moja.

Kwahiyo hapo lazima ujue unataka jeans quality ipi na utaiuzaje.

Ila hapo uliposema hautaki mtumba ndio changamoto. Nashauri upoteze kama siku 3 kwenda Kariakoo kutafuta maduka ya jeans ya wachina. Kuna uzi humu unasema machimbo ya Kariakoo unaweza usoma hapa chini

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Kuhusu mtaji hapo itategemea na wewe unataka nguo ngapi za kuanzia.

1. Size tofauti tofauti lets say size 10 kila size jeans kadhaa.

2. Rangi tofauti tofauti, lets say rangi 10 kila rangi ina size jeans kadhaa.

3. Style tofauti tofauti, kila style ila rangi kadhaa, na kila rangi ina size kadhaa.

Kwahiyo kwa kuanzia unakuta una jeans 100-200 hivi.

200 mara 10k ni kama Mil 2.

Ni mahesabu ya excel sio uhalisia.
 
3. Nashauri uwe mtu wa kwenda na fashion sana kujua hawa viumbe wanataka nini. If possible shauriana na mwanamke au mke wako ambae anapenda sana fashion. Pia fanya research kwenye social media wale wanaouza izo nguo uone trend.

Pia usiuze jeans tupu, ongezea ata t-shirt au tops kadhaa, simple open shoes mikoba ata michache, maana mteja akija ndani anaweza akakosa jeans ila akanunua ata pochi ya afu 5 hawajuagi wanachotaka hawa.

Jitandaze mitandaoni, jaribu kua cheap kuliko wengine na usianze kwa kukodi mahala pa gharama kodi usije umia. Hao wakina Vunja Bei, Frank Knows, Sharobaro.. waliamza mdogo mdogo sana. Usije weka millions kwenye biashara hafu ukafail ukalia na kusaga meno.

Na mwisho mteja hatongozwi kama wanavosema wadau. Maana watakuja watajaribishia jeans mbele yako kama kibolo dinda utafirisika.
 
Ushauri murua

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Kaka madmax asante sana kwa ushauri mzuri
 
Mtaji 10ml-20ml
Midoli yenye shepu elfu 60 kkoo.
Biashara hiyo inahitaji matangazo. Kama biashara zingine za nguo. Ni biashara nzuri sana.
Pata location inayofikika. Wala usiogope wala kujificha wateja wapo tu.
Jeans zipo kkoo. From chambuu mpaka custom made mfn. Fashionova. Yapo machimbo mengi tu ya jeans za kike.

MACHIMBO.
Congo na narung’ombe ndio mitaa ya jeans nyingi.
Bei za jumla
13,14,15

Plus to add up.
Kkoo watu wa jeans
Kuna princess jeans, recho pambakali. Hawa utapata jeans za kisasa zaidi maana wanaagiza.
Mtaji wako haswa ni midoli.
Uwe na midoli mingi. Udisplay nguo zako.
 
Asante sana kwa mchanganuo
 
Asante sana kwa ushauri mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…