Naombeni msaada kwenye hili

Naombeni msaada kwenye hili

mniga

Member
Joined
May 31, 2011
Posts
12
Reaction score
4
Habari wanajamvi.

Nimekuwa nikikabiliana na woodworms (wood borers) kwenye miti na mbao hasa ni wale long-horn beetles wadudu wanao kula mbao kwa muda mrefu kwa kutumia aina tofauti todfauti ya viuatilifu ikiwemo Dichlorvos(DDV), Chloropyrifos(Colt) na Imidacloprid (Twiga Prid) bila mafanikio.

Nimeshauriwa nitumie kiuatilifu chenye permethrine EC 25% kama kuna anyefahamu inapouzwa hapa Tanzania anijuze ama ushauri na nini nitumie ili kumaliza tatizo. Ahsante.

IMG_20231107_055526_244.jpg
 
Habari za leo. Mbao ni kwa ajili ya matumizi gani. Na wingi wake ni kiasi gani.
 
Ukitumia kiuatilifu cha aina moja kwa muda mrefu wadudu wanajenga usugu.
Pili, kujua matumizi.ni.muhimu usijekuta unajengea mzinga wa nyuki au kutengeneza vyombo vya kulia.chakula.
 
Tumia dawa ya Mida 200SL kutoka ya Kampuni Osho Chemical Industries Ltd yenye active ingredient Imidacloprid 200g/l
 
Tumia dawa ya Mida 200SL kutoka ya Kampuni Osho Chemical Industries Ltd yenye active ingredient Imidacloprid 200g/l
Habari, nilitumia dawa tajwa baada ya siku mbili wadudu walikuwa kmya ila baada ya hapo nawasikia kila siku. Je nirudie tena dawa ama nifanye nini? Leo ni siku ya kumi tangu mipige dawa.
 
Habari, nilitumia dawa tajwa baada ya siku mbili wadudu walikuwa kmya ila baada ya hapo nawasikia kila siku. Je nirudie tena dawa ama nifanye nini? Leo ni siku ya kumi tangu mipige dawa.
Vipi mniga ulipata ufumbuzi? Nami napitia janga hili.
 
Salama,Hapana bado.
Dah, Paa lako liko wazi au umeweka gypsum/ceilingboard? Unaweza kuondoa mbao zilizoathirika? Nadhani hii ndio njia sahihi ya kumaliza tatizo. ila kwangu itakua ngumu kuondoa mbao bado naumiza kichwa
 
Dah, Paa lako liko wazi au umeweka gypsum/ceilingboard? Unaweza kuondoa mbao zilizoathirika? Nadhani hii ndio njia sahihi ya kumaliza tatizo. ila kwangu itakua ngumu kuondoa mbao bado naumiza kichwa
Mimi pia nshaweka Gypsum
 
Back
Top Bottom