Naombeni msaada wa dawa ya Kichefuchefu

Hii hata Mimi naijua huwa naitumia inasaidia sana.inatakiwa katikati ya kiganja baada ya kusugua kwapani.sio kwamba kusugua kwapani mpaka uvue nguo,Bali sugua hivyo hivyo hata bila kuvua nguo

Dawa ya kichefuchefu nusa tu harufu ya kikwapa dakika moja kikwapa chako njoo utupe mrejesho mm ndo dawa nayotumia nikipata hilo tatizo na hata wazee wa zaman ndo ilikua dawa yao hio

Ni kweli, mimi hunisaidia sana, hata kwa kunusa kwapa bila kusugua na mikono, kichefuchefu huwezi kujisikia tena kwa wakati huo.

Ukiwa umekaa sugua kwapa la kulia na mkono wa kushoto.kisha wavkulia kwapa la kushoto mkono wa kulia.kila umalizapo mkono unuse

Duh, kumbe watu wengi mnaijua hii dawa!

Yaani nilikuwa napitia uzi nione kama hakuna aliyetoa hii dawa niitoe fasta, hivi mliijuaje nyie?

Maana hii dawa ni kiboko ya kichefu chefu.

Halafu huwa najiuliza kama ukitumia kikwapa cha mwenzako utapona pia?
 
Uko katika kikao au daladala,utaweza kufanya hivyo?na je kwa sisi wengine tunatumia manukato au perfume kwa wingi,unakuta kwapa lote ni harufu ya manukato
 
Uko katika kikao au daladala,utaweza kufanya hivyo?na je kwa sisi wengine tunatumia manukato au perfume kwa wingi,unakuta kwapa lote ni harufu ya manukato

Kwenye daladala unafanya kwa chati, unaweza kuingiza hata kidole tu kwenye kwapa, unakisugua kinapata ile harufu halafu unakinusa, bila hata mtu kujua unafanya nini.

Kwenye habari ya kutumia manukato sasa hapo sina jibu, ila ukisugua ile harufu utaipata tu.
 
hii ndo tiba rahisi sana kwa wakati mfupi lakini. ukijisikia kichefuchefu lala chali lazimisha ubongo wako ulale kitaacha fasta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…