Naombeni msaada wa haraka jamani, vinginevyo naumbuka

Naombeni msaada wa haraka jamani, vinginevyo naumbuka

Jamani nipo hapa magomeni usalama kisuma bar nimekuja na Dada zangu wametoka mpwayungu dodoma nikawaambia waagize vinywaji mm naenda toilet.

Sasa chakushangaza nimetoka maliwato Ile nafika wote wawili wameagiza savanna nane yaani kila mtu nne nne. Nimepigwa na butwaa maana hivi vinywaji imported hapa kisuma ni 5000 namm nimekuja na hela ya eagle na pliziner tu vinginevyo hii ni kesi. Sasa nimekuja haraka humu jukwani center of intelligence mnipe ushauri wa haraka vinginevyo tutaitwa vibaka hapa.
Waambie wazirudishe fasta
 
Heri nusu shari kuliko shari kamili mkuu maana hapo hakuna namna. Mimi niliwahi kuwapeleka watu shoppers wakashop vitu almost vya laki sita ilikiwa aibu pale kaunta. Yani ilikuwa kituko haswaa
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Ulifanyaje kujinasua kwenye huo mtego
 
Hahahaha inaonekana slay queen wako na genge lake walikunyoosha mjuba😅
🤣🤣🤣 Mjuba slay queen wapi, watu wametoka huko mkoani ndugu nikasema twende na nyinyi msukume vitorori. Wee walijaza ule mtorori mkubwa kufika kaunti kila akipitsha barcode reader naona pesa inasoma tu nikiangalia torori bado limejaa mara laki sita jasho linanitoka. Dah ilikuwa aibu sema nilitoka nje nikachukua ela atm nikalipa ila nilikuwa sizungumzi njia nzima mpaka tunafika tegeta.
 
Hahahahah wananchi wamesukuma kitololi kweri kweri😅 wakihisi wewe ni kama Drake kwenye Gods plan video!
 
Back
Top Bottom