Naombeni msaada wa hii ndoto yangu inayojirudia rudia

Naombeni msaada wa hii ndoto yangu inayojirudia rudia

Mshana usiwadanganye watu.Hii ndoto ni michezo ya kichawi anayofanyiwa huyu jamaa.Na kumwambie alale na mifuopa au apake mafuta ya nguruwe ni kumdhalilisha tu.Shetani hamwogopi nguruwe.Jibu la tatizo hili ni kuishi maisha matakatifu ndani ya Yesu ili Shetani asiweze ku,kuchezea.Full stop.

Umenena vyema ndugu. Kuna msemo unasema "You can not solve a problem by the same methods that created a problem"

Mel James uko kwenye vita vya Kiroho ndugu yangu na ushindi wake unapatikana tu kama utapambana kiroho....rejea Efeso 6:11-18.

Usiogope wala kutetereka kwasababu Kristo aliushinda ulimwengu. Akiwa ndani yako nawe utashinda Wafilipi 4:13

Omba bila kukoma, tubu na Yesu atakuokoa from your attackers.
 
Hiyo ni michezo ya wanga wanakulisha ngozi za wanyama most likely fisi,cha kufanya lala na mfupa wa kitimoto au pakaza mafuta yake kitandani au ukiweza jipake mwilini wakati wa kulala
Sidhani kama mfupa wa na pia kitimoto ni tishia kwa hao jamaa kama sio mapepo; waweza kulala nao na ukasikia maneno haya, "kaongeze nyingine ..." Jitoe kwa Bwana moja kwa moja, maana kwa kusudi hili Yesu alifunuliwa ili apate kuziharibu kazi za shetani, mojawapo ikiwa ni hiyo ya wewe kupata shida.
 
....kuna kitabu fulani kina kava jeusi.....kitabu hiki kilimshangaza mfalme wetu baaada ya kusaidia mambo mengi...jaribu uwe unakiweka chini ya mto wakati wa kulala......manake waweza kuwa mvivu kukisoma.......
Kuweka kitabu chochote chini ya mto hata kama ni Biblia yaweza kutumika kama hirizi, ha sie hatujaamuliwa kuwa na imani katika kitabu bali katika maneno ya Bwana yaliyomo ndani yake
 
Kuweka kitabu chochote chini ya mto hata kama ni Biblia yaweza kutumika kama hirizi, ha sie hatujaamuliwa kuwa na imani katika kitabu bali katika maneno ya Bwana yaliyomo ndani yake

Ni kweli ndugu, wote tumetoka mbali hata mimi nilikua nikiamini kuwa ukilala na Biblia unaongeza ulinzi dhidi ya nguvu za giza.

lakini nilikua nakosea, yamkini vitu vingine tuliaminishwa angali watoto (kiroho). Ila anavyosema ndugu Mwenechu ni sawa kabisa. Tuepuke Imani hizi zisizo na msingi.
 
Mungu awabariki kwa msaada mzuri wa mawazo mlionipa. Nashukuru sana pia kunitia moyo kuwa problem itakuwa solved kwa kusali.
 
Mkuu, unalishwa nyama za watu usiku. Unahitaji maombi.
 
Mshana usiwadanganye watu.Hii ndoto ni michezo ya kichawi anayofanyiwa huyu jamaa.Na kumwambie alale na mifupa au apake mafuta ya nguruwe ni kumdhalilisha tu mwenzio.Shetani hamwogopi nguruwe.Shetani anamwogopa Yesu tu.Kwahiyo jibu la tatizo hili ni kuishi maisha matakatifu ndani ya Yesu ili Shetani asiweze kumchezea.Full stop.

Sidhani kama mfupa wa na pia kitimoto ni tishia kwa hao jamaa kama sio mapepo; waweza kulala nao na ukasikia maneno haya, "kaongeze nyingine ..." Jitoe kwa Bwana moja kwa moja, maana kwa kusudi hili Yesu alifunuliwa ili apate kuziharibu kazi za shetani, mojawapo ikiwa ni hiyo ya wewe kupata shida.

Ni rahisi sana kumshauri mtu aishi maisha matakatifu na kumpokea Yesu kama vile ni kitu rahisi sana....this is too passive....maneno ya Mungu yanasema hivi ...'Tazama WOTE wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa mungu...' Sasa unapomdanganya mtu aishi maisha matakatifu....hivi tuna matakatifu kweli dunia hii? Utakatifu ni level ya juu mno jamani....mwanadamu na changamoto za dunia hii na uchafu wote alionao haweza kuwa MTAKATIFU hata mara moja

Ni kweli kabisa Yesu Kristo ni kiboko ya shetani lakini ni mpaka umjenge mtu kiimani hasa...tunachotafuta na ufumbuzi wa haraka kwanza...mtu anakuja kwako na shida kama hiyo, unamsaidia kwanza kuondokana na tatizo kwanza kisha ndio unakuja kumjenga kiroho

Kingine na cha muhimu sana, kumpokea Kristo haimaanishi kuwa ndio umemuepuka shetani, la hasha tena ndio kwanza atakuja kwa nguvu zaidi akitaka urudi kwenye himaya yake, kwahiyo waliookoka wako kwenye risk kubwa ya mapigo ya shetani kuliko asiye okoka
 
Usihangaike tafuta mafuta ya zeituni (vargin olive oil) wengine wanayaita mafuta ya upako . .. Tone Moja tu kwenye paji la uso kabla ya kulala ...
 
Inawezekana una tatizo la kusaga meno (bruxism) ukiwa umelala ndio maana ukiamka meno yanakuwa na maumivu, jaribu kumwona daktari.

Lol the only medical explanation the entire thread. Wabongo washirikina duh!
 
Kufuatana na Biblia kuna ndoto za aina tatu (nimekopi sehemu)
(a) Kuna ndoto kutoka kwa Mungu. Soma kitabu cha Hesabu 12:6, na Yoeli 2:28.​
(b) Kuna ndoto zinakuja kwa sababu ya shughuli nyingi. Soma kitabu cha Mhubiri 5:3.​
(c) Kuna ndoto za uongo zinazotoka kwa shetani aliye baba wa uongo. Soma kitabu cha Yeremia 23:52 na Yohana 8:44.
Tafuta msaada kwa kufuata imani yako ya kidini.​
 
1. Ukiota unahesabu hela
Hii inamaanisha kwamba nyota yako ya UTAJIRI imeshaibiwa na wachawi.

2. Ukiota unawaona watu waliokwisha kufa zamani
Hii inamaanisha tayari na wewe unaandamwa na ROHO YA MAUTI, unatafutwa kuuawa kwa namna yoyote.

3. Ukiota umeyarudia maisha ya utotoni, shule ya msingi au sekondari wakati ulihitimu chuo kikuu zamani
Hii inamaanisha unafuatiliwa na ROHO YA KUANGUKA, hii ni dalili ya kufungwa na roho za mizimu na mababu.

4. Ukiota unafukuzwa na maadui
Hii inamaanisha WACHAWI WANAKUTUMIA kwenye mambo yao pasipo wewe kujijua.

5. Kuota unakula/ kulishwa vyakula usingizini/ ndotoni
Hii inamaanisha UMEPANDIKIZWA ROHO ZA KICHAWI na za mizimu mwilini mwako.

6. Ukiota Unafanya mapenzi
Hii inamaanisha UNAMILIKIWA NA MAJINI MAHABA, na hiki ndicho chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika na wengi kuwa na tatizo la utasa na hata wanawake kutoolewa kabisa.

Pale unapoota ndoto za namna hii na zile ambazo sikuzitaja, basi ujue unahitaji maombi ya UKOMBOZI kwani hiyo ni dalili ya kufungwa na NGUVU ZA GIZA.
 
Naomba kuuliza nifanyaje nimjue anayenilisha mazaga usiku bila kwenda kwa mganga? Nimfuate mchana tukayajenge.
 
Ndoto hazina uhalisia na maisha bali ni mrejesho wa fikra na shughuli ambazo huwa zinachukua mda mwingi wakati wa mchana katika pilikapilika zako.
 
Back
Top Bottom