Naombeni msaada wa hili la kutopigia ndugu simu

Mimi nishasemwa sana ila ni bora kuwa kimya kuliko kunafikiana. Tunawasiliana kwa jambo muhimu tu. Huwa nashangaa wanaolalamikiaga ndugu kuwa hawawatafuti.
 
Kama huwapigii wakupigie wao. Achana na watu wanaojiona wao ni muhimu kuliko wengine
 
Ndugu unafki mwingi sana + kusemana semana hovyo Tabia za kiswahili hayo mambo yamenishinda so nikaamua kujiweka kando nao kabisa
Umefanya vyema kwa minajili ya amani yako ya moyo mkuu.
 
Nilishapotezana na ndugu katika simu tangu zamani na niko poa. Hii ni baada ya kugundua kuwa ni afadhali uishi kamanyama kuliko kujiconect na watu wasiokuheshimu.

Nilizaliwa mwenyewe, nitakufa mwenyewe, na nitazikwa mwenyewe.
Sorry bro pande ipi ya asili ni South North East au West mwa Tanzania? Kwasababu nina rafiki zangu wengi sana wametoka upande flan wanalalamika sana kumejaa watu wenye dharau kwa ndugu zao
 
Mi pia ndo sipokei kabisaa,,nikikuhitaji ntakupigia
 
Siku hizi napiga. Watu wanafurahi ukiwapigia, nimeamua kusambaza furaha.
 
Sorry bro pande ipi ya asili ni South North East au West mwa Tanzania? Kwasababu nina rafiki zangu wengi sana wametoka upande flan wanalalamika sana kumejaa watu wenye dharau kwa ndugu zao
North
 
Mimi mpaka leo wananilaumu siwapigii simu. Na mimi siwezi kubadilika wataongea watachoka
Actually nawahurumia wanavyolalamika lakini sasa huyu ndio mimi. Siwezi kuwa kama wao. Kwani nisipowapigia wanapungukiwa nini?
Mimi nikiamua kuwapigia ndugu simu huwa naomba wasipokee. Ila bahati mbaya nikisema nijaribu tu kuwapigia kimzaha mzaha wanapokea kweli 🀦
 
Yaani mimi ni introvert VIP hali yako mbona kidogo nje ya Bi mkubwa Mara moja moja ndugu wengine wanajua na exist kwenye Dunia na hawajui naishije!
 
Hata mm nipo hvy na hua wananilalamikia sana kwa tabia hiyo, ila nilichogundua n vile mnakuwa mbali hvy hakuna vile vitu vya kuwafanya mzungumzie sana hvy hata mazoea yanapungua
 
Kimsingi hakuna wa kunipa ugonjwa maana nimeshajifunza kutokumbatia mtu asiyenithamini.
 
Mazoea sana na kujuliana hali mara kwa mara huleta kudharauliana!, bora kupiga kimya wasikujue sana kiundani.
 
Mungu anisamehe hii kitu usiponipigia imeisha huu mwaka mpya ndugu zangu hata kuwatakia heri ya mwaka mpya nimeshindwa

Na dakika sijawahi kosa
Muda sio tatizo
Ni roho flani ambayo binafsi siipendi ila kubadilika nashindwa

Nilipojiunga chuo nimefika nimekaa miez sijapitia mtu mpaka nilipopigiwa na wao wenyewe

Na hata kuomba mtu hela siwezi hata kwa ndugu nikwame nife tu ila mtu akiniomba ni mepesi sana kutoa msaada ila mi sinufaiki na misaada hata napo kuwa nimekwama


Mungu basi tu
 
Tupo wengi ndgu yangu, ila nashukuru wengi wao wamezoea.

Na hizi whatsapp status siku hizi zinasaidia, nikiona status zao ni salamu tosha maana mimi huwa siweki hata hizo status.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…