Mimi naomba nikuulize swali hapa mkuu.
Wakati ukimwi unaingia TZ ulianzia Kagera. Wakati huo hakuna aliyekuwa na taarifa juu yake. Watu wakaunasa wakakonda wakaisha hadi wahaya wakauita slim kutoka neno la kingeereza kwa kuwa watu walikuwa wanakonda mtu hata akilala kitandani haonekani.
Lakini wakati huo hata ARV hazikuwepo, so watu hawakuwa wakitumia ARV lakini bado walikonda na wakafa. Kuna maeneo kama kiziba hadi nyumba zilifungwa unakuta mama, baba, mjomba wamekufa wote.
Sasa kitu gani kilifanya watu wapukutike wakati ARV hazikuwepo?
Na baada ya ARV kuwepo watu wakapungua kufa na wengine wakaishi na kufa wakiwa na miili yao.
Nina kaka yangu huu ni mwaka wa 17 anatumia ARV and yuko poa huwezi hata jua.
Nachotaka unieleweshe, ni kwanini kabla ya ARV ambayo umadai ni sumu bado watu walikuwa wanakonda na kufa vibaya sana.
Mind you siko hapa kukupinga ila nataka nipate elimu