Kuna wanandoa wametangana, sasa walifanikiwa kupata mtoto ambae ana umri wa miaka 2, chanzo cha wa kutengana kwao wanakijua wao ila mwanaume analalamika kuwa mke wake anampenda ila sasa hajatulia halafu anamdharau kwakuwa hana kipato.
Sasa mwanamke hampatii hata kidogo mwanaume nafasi ya kuwa na mtoto, ingawa anaelewa kwa sasa mtoto anatakiwa akae na mama yake, huyu mama amekuwa akimtumia mtoto kama njia ya kumkomoa mumeo na kuonyesha hasira zake.
Hapa sheria iko vipi? na huyu mwanaume afanye nini ili aweze angalau kupewa muda wa kumchukua mtoto na kukaanae angalau siku 2 au tatu, sababu jamaa hajaoa tena na anaishi na ndugu zake.
Naomba msaada wa kisheria na jinsi ya kuwasiliana na mwanasheria wa ustawi wa jamii ili nimsaidie jamaa awe salama na apate kinga kwa maisha yake juu ya mwanae kwa baadae.
Asanteni.