Naombeni msaada wa kitaalamu

Naombeni msaada wa kitaalamu

Michael Anthon

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2017
Posts
219
Reaction score
108
Samahanini kama haitaleta mashiko kwenu ila mwenzenu naombeni msaada wakimawazo kwa wenye utaalaumu humu ndani

Ndugu yangu ana tatizo la kusinzia muda wote haijalishi usiku analala au laah anapokaa tuu hasa kama wakati wamchana basi yeye hachelewi kulala utakuta mnaongea ukijiziuka kidogo utajikuta unaongea peke yako ananishangaza wakati mwingine hata akiwa anatembea basi anatembea huku anasinzia najiuliza niusingizi gani huu usio isha?

Je kama niugonjwa basi naombeni kufahamisha ugonjwa huu unaitwaje na unasababishwa na nini? Alizaliwa safi na alikuwa mchangamfu sana lakini toka 2006 tatizo hili lilipompata hana uchangamfu ule wamwanzo jinsi ugonjwa huu ulivyoanza ilikuwa jioni moja tukiwa katika mlo wa jioni kijijini huko namtumbo gafla tukaona mwenzetu anaweweseka nakupoteza fahamu toka hapo ni kusinzia tu mpaka leo hivyo kama kuna anaejua ugonjwa huu na namna ya kutibia atakuwa amenisaidia asanteni
 
Ni kweli mtu anaweza kutembea huku analala...!?
Ebu fafanua vizuri hapa..
 
Ni kweli mtu anaweza kutembea huku analala...!?
Ebu fafanua vizuri hapa..

Inawezekana nishawahi kushuhudia kijana mmoja wa kutoka huko huko Namtumbo nilikuwa nimmezidi darasa moja enzi hizo pale Kibaha Sec alikuwa na tatizo kama hili, Ishawahi tokea kuna siku karudi bwenini kutoka darasan baada ya masomo amekaa kitandani kwake ili abadili nguo,mara akalala wakati suruali anayoichojoa iko nusu magotini tuu.

Kuna watu walisema labda ni ugonjwa wa malale unaosababishwa na mbung'o
 
Amshukuru mungu tu sababu kuna wengine wanatamani kulala ata kwa sekunde lakini wanashindwa
 
1. Halali usiku.

2. Mawazo mengi.

3. Lishe duni.

4. Sleeping sickness/ trypanosomiasis .

5. Kuna dawa za muda mrefu anazotumia.

6. Kuna ugonjwa wa muda mrefu anaoumwa mfano wa moyo nk.

sasa we angalia lipi ninamuhusu hapo.
 
1. Halali usiku.

2. Mawazo mengi.

3. Lishe duni.

4. Sleeping sickness/ trypanosomiasis .

5. Kuna dawa za muda mrefu anazotumia.

6. Kuna ugonjwa wa muda mrefu anaoumwa mfano wa moyo nk.

sasa we angalia lipi ninamuhusu hapo.
Sijui kama nitakuwa nimeeleka vizuri hakuwa akisumbuliwa na homa yoyote kabla wakati tatizo hilo linaanza alikuwa na umri wa miaka 10 mpaka leo bado analo na nimeeleza kuwa analala mchana na usiku yeye usingizi haumwishi na nikijana mwenye afya nzuri tuu tatizo hili lilimpelekea mpaka mwalimu wake amkatishe masomo maana hakuwa akiweza kuhimili kukaa bila kusinzia nakama ni mawazo mtoto wamiaka hiyo mawazo apate wapi? Kapimwa mara kadhaa kwa hospital za kule kwetu Ruvuma hawakugundua lolote
 
Back
Top Bottom