Typhoid
JF-Expert Member
- Feb 7, 2012
- 226
- 70
Mama yangu anasumbuliwa na ini(liver), limevimba na ukimuona amekonda sana, mwezi 11 alifanyiwa uchunguzi bugando mwanza na akaambiwa kibofu cha mkojo(galbladder) kina michanga ndani, alifanyiwa upasuaji, ktk maelezo yao walisema kumbe sio kibofu cha mkojo tu ini lote lina matatizo. Baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali hakumaliza wiki akaanza kukonda gafla, tukampeleka musoma hospital, wakakataa hata kumlaza wakampa tu vidonge vya kutumia wakasema hamna namna ya kufanya ini limisha halibika.
Kihistoria mama amekuwa akitumia pombe aina ya gongo kwa mda mrefu sana, nahisi ndo itakuwa imemletea tatizo la ini, pamoja na kuwa hospitali imeshindikana, ningependa kujua kama naweza kupata mawazo juu ya kumsaidia mama, naumia kumuona analia mda wote, kama kuna mtu ana utalaam wowote wa hilijambo naombeni msaada wa mawazo au tiba kama ipo ya hilo tatizo. Asanteni