naombeni msaada wa mawazo wanajf

naombeni msaada wa mawazo wanajf

Typhoid

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2012
Posts
226
Reaction score
70
Mama yangu anasumbuliwa na ini(liver), limevimba na ukimuona amekonda sana, mwezi 11 alifanyiwa uchunguzi bugando mwanza na akaambiwa kibofu cha mkojo(galbladder) kina michanga ndani, alifanyiwa upasuaji, ktk maelezo yao walisema kumbe sio kibofu cha mkojo tu ini lote lina matatizo. Baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali hakumaliza wiki akaanza kukonda gafla, tukampeleka musoma hospital, wakakataa hata kumlaza wakampa tu vidonge vya kutumia wakasema hamna namna ya kufanya ini limisha halibika.
Kihistoria mama amekuwa akitumia pombe aina ya gongo kwa mda mrefu sana, nahisi ndo itakuwa imemletea tatizo la ini, pamoja na kuwa hospitali imeshindikana, ningependa kujua kama naweza kupata mawazo juu ya kumsaidia mama, naumia kumuona analia mda wote, kama kuna mtu ana utalaam wowote wa hilijambo naombeni msaada wa mawazo au tiba kama ipo ya hilo tatizo. Asanteni
 
Pole sana mkuu, nilipokua nasoma hii thread machozi yalikuwa yanalengalenga. Inauma sana kuona mama anapata maumivu na huna kitu cha kufanya.Wataalam watakuja na ushauri wao.

Mimi nnachoweza kushauri hapo ni kumwombea kwa Mungu muweza yote na kwa rehema zake analotaka liwe huwa.
Lisilowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu linawezekana. Mungu amponye.
 
POLE SANA! Liver desease (Hepatic) sio mchezo ! Ila Itategemea sana na stage ya ini lilivyofikia.Hilo inaweza kuwani Toxin Hepatitis (caused by alcohol) ingawa nyingine zinaletwa na viral hepatitis
(caused by virus) na pia kuna ya Hereditary ya kurithi.

Mara nyingi ugonjwa huo huathiri sana mfumo wa usagishaji chakula, matatizo ya kisukari, immune disorder, abnomal absorption of fat, na Je limefikia critical metabolism problem? (Indigestion, reflux, deficity of fat soluble vitamin,Hemorrhoid, gall stone(kama ulivyosema), intolerant to fat food, intolerant to alcohol, kichefuchefu kutapika, kuvimba tumbo, na constipation).

Vipi nerve system disorder?(like recurrent headache, overheating, nause etc

Pole sana ndugu yangu. Kama halijafikia hatua mbaya sana,ila wanashauri Cut out alcohol, Improve diet na reguler exercise kutegemeana na hali ya mgonjwa.

kama ni Cirrhosis stage inatesa sana kwa mgonjwa wa ini.
 
Typhoid, hili jina limenishtua kidogo..

POLE kwa matatizo ya mama,

Ni vizuri kujua Umri, Uzito wa mama kabla ya yote na ningependa kusahihisha kuwa gall bladder(ni mfuko wa nyongo) na Urinary bladder ndiyo kibofu cha mkojo.

Pia kubla ya kushauri ni vizuri kujua uwepo/kutokuwepo kwa dalili nyinginezo mfano;
-Tumbo kujaa/kuvimba, Miguu kuvimba/kufura,
-Je kuna dalili ya "kuchanganyikiwa" kuongea/kutamka mambo yasiyoeleweka kwa wengine wakati fulani,
-Choo, mkojo kuna tofauti yeyote kati ya alivyokuwa zamani na sasa?

Na je, mama alitumia pombe kwa muda gani?Anaendelea kutumia bado?Kama ndiyo kwa kiasi gani?

Ni tiba gani uliyopata( yaani unaweza kukumbuka jina la dawa/vidonge mama alivyopewa) ? na hali ilikuwaje baada ya kuvitumia?
-Ni lishe ya nanna gani aitumiayo sasa mama?

Again, Pole.
 
Last edited by a moderator:
Typhoid, hili jina limenishtua kidogo..

POLE kwa matatizo ya mama,

Ni vizuri kujua Umri, Uzito wa mama kabla ya yote na ningependa kusahihisha kuwa gall bladder(ni mfuko wa nyongo) na Urinary bladder ndiyo kibofu cha mkojo.

Mama ana miaka 65, mpaka sasa ana uzito wa kilo 42

Pia kubla ya kushauri ni vizuri kujua uwepo/kutokuwepo kwa dalili nyinginezo mfano;
-Tumbo kujaa/kuvimba, Miguu kuvimba/kufura,
-Je kuna dalili ya "kuchanganyikiwa" kuongea/kutamka mambo yasiyoeleweka kwa wengine wakati fulani,
-Choo, mkojo kuna tofauti yeyote kati ya alivyokuwa zamani na sasa?

Kwa kweli tumbo linajaa sana, limevimba kiasi kwamba mwili wote unaona tumbo pekee, ana miezi2 hali chakula chochote, anakunywa uji peke yake, kwa kweli haonyeshi dalili ya kuchanganyikiwa, anaongea vizuri tu, na huwa anaomba apewe dawa ya kuharisha ila wanamkatalia. Anakojoa mkojo wa njano siku zote tangu aanze kuugua.

Na je, mama alitumia pombe kwa muda gani?Anaendelea kutumia bado?Kama ndiyo kwa kiasi gani?

Mama ametumia pombe kwa mda mrefu sana, ni zaidi ya miaka 30.
Ni tiba gani uliyopata( yaani unaweza kukumbuka jina la dawa/vidonge mama alivyopewa) ? na hali ilikuwaje baada ya kuvitumia?

Mimi nawasiliana na ndugu zangu ili waweze kunipa jina la dawa anazotumia kwa sababu siko nyumbani mda huu.

-Ni lishe ya nanna gani aitumiayo sasa mama?

Ni kama nilivyosema hapo juu anakunywa uji peke yake sasa.

Again, Pole.
Asante, na samahani kuchelewa kujibu.
 
Back
Top Bottom