Naombeni msaada wa ushauri kati ya Kuroiler na Broiler.

Robb

Member
Joined
Jan 16, 2013
Posts
61
Reaction score
84
Nimejaribu kupitia pitia humu kuhusu ufugaji wa hizi aina mbili za kuku nimegundua yafuatayo.

Kwa upande wa broiler nimegundua kuwa wanahitaji umakini wa hali ya juu haswa kwenye chakula wanahitaji chakula maalum cha kiwandani au kitengenezwe na mfugaji kwa formula inayotakiwa na watakula mwanzo hadi mwisho wanapotoka kwa ajili ya soko pia wanahitaji usafi huku upande wa Kuroiler nimesikia wao huwa wala starter kipindi cha mwezi wa kwanza na mbeleni unaweza endelea kuwapa chakula kama cha kuku wa kienyeji wa kawaida na kwa kuongezea hawa unaweza kuwafuga kwa free range.

Kwa upande wa changamoto nilizozisikia ni kwamba kwa upande wa broiler risk iliyopo ni endapo utachelewa kupata soko basi kuku wataendelea kula mtaji sababu itabidi wanunuliwe chakula wakati washafikisha muda wa kutoka ila pia upande wa Kuroiler nimesikia wafugaji wanalalamika humu kuwa kuku mpaka wanafikia miezi 6 hawajaanza kutaga au bado hawajakua vizuri kufikia ukubwa wa soko je hapa kwa kesi kama hii ya hawa kuroiler ndio lile tatizo la kusema inatakiwa upate vifaranga vya F1??? Ingawa kwa muda huo huo nimesikia tena vifaranga vya F1 vya kuroiler ni bei ghali tofauti na vifaranga hivi vya mtaani ambavyo bei yake mara nyingi ina range Tsh 2300 - 2700.

Najua humu tuna wafugaji wengu tu hivyo basi naomba nipate ujuzi wenu enyi wafugaji mliomo humu kati ya broiler na Kroiler ni aina gani nzuri ya kuanzia ufugaji maana sina ujuzi wa ufugaji zaidi Mbwa na kuku wa kienyeji wale wa nyumbani ambapo ufugaji ule sio wa kibiashara, Nataka nianze vifaranga angalau 200 nipate ujuzi kwanza halafu baada ya hapo niongezee mpaka kufika vifaranga 1000.
 
Kama ni mwanzo anza na mia moja broiler maana ndani ya mwezi unakuwa umemaliza biashara lakini hawa kroiler au chotara unafuga mda mrefu sana wanahitaji mtaji maana kuna dawa na chakula ndani ya miezi mitano ni mzigo hata kama baadae watakula pumba.
 
Asante kwa ushauri mkuu, na hawa Kuroiler mpaka wakomae ni miezi mitano?? mbona huwa wanasena wanachukua miezi 4 hadi kuku au ndio lugha za wafanyabiashara ili wauze vifaranga vyao???
 
Kwa nijuavyo:
Kuroiler wa nyama anakua tayari kuanzia umri wa miezi 2.5 - 3.
Wale wanaowekwa kwa ajili ya mayai wanaanza kutaga kuanzia miezi 4.5, 5 na 6.
Kwanini kuna tofauti?

Matunzo katika ujumla wake huathiri sana kuanza kwa utagaji (onset of laying).
Mwanga huathiri pia kuanza utagaji na utagaji wenyewe.
Kuwepo vipindi tofauti vya mwanga hasa wa jua "Photoperiodism".
Kwa wale wanaopata vipindi viriefu vya mwanga huwai kutaga tofauti na wale wanaopata vipindi vifupi vya mwanga, na hata pale vipindi vya mwanga vinapobadikika huathiri pia utagaji, hasa kupunguza kwa wale waliokwisha kutaga.

Aksante.
 
Ahsante kwa somo mkuu, umesema wa nyama huwa wanakuwa tayari kuanzia miezi miwili na nusu hadi mitatu?? Mbona kuna mfugaji mmoja nimeona kuku wake aina hiyo hiyo ya kuroiler wana miezi mitatu ila kwa kweli kimuonekano bado ni wadogo sizani kama wanafaa kwa ajili ya soko, tukilinganisha na ulivyosema je yawezekana labda ni sababu ya matunzo duni au???
 
Matunzo duni ni moja ya sababu lakini pia uzao pia ni sababu ingine.
 
Kwa nijuavyo:
Kuroiler wa nyama anakua tayari kuanzia umri wa miezi 2.5 - 3.
Wale wanaowekwa kwa ajili ya mayai wanaanza kutaga kuanzia miezi 4.5, 5 na 6.
Kwanini kuna tofauti?

Matunzo katika ujumla wake huathiri sana kuanza kwa utagaji (onset of laying).
Mwanga huathiri pia kuanza utagaji na utagaji wenyewe.
Kuwepo vipindi tofauti vya mwanga hasa wa jua "Photoperiodism".
Kwa wale wanaopata vipindi viriefu vya mwanga huwai kutaga tofauti na wale wanaopata vipindi vifupi vya mwanga, na hata pale vipindi vya mwanga vinapobadikika huathiri pia utagaji, hasa kupunguza kwa wale waliokwisha kutaga.

Aksante.
Kuroiler miezi 2 wanakuwa tiyari? Mh,
 
Piga gharama ndo suluhisho. Fanya mahesabu ya kufuga either Kuroiler kadhaa kama.300 au Broiler 300.

Bila kufanya mchanganuoa.utakuwa.unajidanganya.

Lazima.ujue cost na.pia pay back.period.kwa.kila aina
 
Kweli hilo nalo wazo zuri mkuu, ila kwa hesabu za haraka haraka pay back period ya broiler ni nzuri kuliko ya Kuroiler ila kwa cost of operation kwa sijajua ipi itakuwa na cost kubwa, ngoja nijaribu kupiga hesabu.
 
Zthread nzuri sana hii kwa wafugajj serious kuna kitu cha kujifunza hapa ... nakushauri kwanza anza na pilot project kuku wachache wa kuroiler let say 50 birds na Broiler wachache pia batch ya 200 birds .... utaweza kumudu gharama ya kuwafuga kwa ufanisi ili kupata mavuno yaliyo bora .... halafu hapa unaweza ku-test market bila panic na kupata uzoefu wa changamoto kama magonjwa

ukiweza kufanikiwa kufuga Kuroiler semi free range utapata mavuno mazuri sana kwani utauza mayai na kuku atauzika vizuri kama wa Kienyeji .... high yield

all the best mkuu
 
Thread nzuri sana hii kwa wafugajj serious kuna kitu cha kujifunza hapa ... nakushauri kwanza anza na pilot project kuku wachache wa kuroiler let say 50 birds na Broiler wachache pia batch ya 200 birds .... utaweza kumudu gharama ya kuwafuga kwa ufanisi ili kupata mavuno yaliyo bora .... halafu hapa unaweza ku-test market bila panic na kupata uzoefu wa changamoto kama magonjwa

ukiweza kufanikiwa kufuga Kuroiler semi free range utapata mavuno mazuri sana kwani utauza mayai na kuku atauzika vizuri kama wa Kienyeji .... high yield

all the best mkuu

Ahsante kwa ushauri mkuu, hili wazo zuri sana pia, Nilipanga pia nianze na pilot project kwanza ingawa mpaka sasa nimeona broiler return yake inaonekana haraka nitaanza nao hao halafu nitatafuta na kuroiler kadhaa niwafuatilie ukuaji wao na running cost yao hadi kuwa tayari kwa ajili ya soko maana me lengo langu ni kufuga kwa ajili ya nyama sio mayai.
 
Me nakushauri anza na Kuroiler kwanza ghalama zake za ufugaji zipo chini kuliko Broilers.

Kama ukiwa smart katika project yako utapiga pesa balaa.

[HASHTAG]#broilers[/HASHTAG] anakula chakula maalamu kutoka kiwandani anatakiwa ale masaa 24 ndani ya weeks 5~6 mwanga bandani uwe wa kutosha muda wote.

Kila wanavyokua ndipo wanapo ongeza kasi ya kula watakapo fikisha weeks 5 kama soko likiwa halipo vizur watakula hadi mtaji kwasababu katika kipindi wanakula sana. Utakapo panic usipo wapa chakula vizur wana-slop yani wanakua wepesi.

[HASHTAG]#ndani[/HASHTAG] ya hizo weeks 5 unawauza kwa bei ya 5500-6000: ukipiga hesabu kila kuku kala 4000 pamoja na madawa, Boost nk faida inaweza ikawa 1500 mwisho 2000 kwa kila kuku.

kama ukiwa na kijana wa kazi unatakiwa umlipe, umeme nk.....

kuku chotara wakiwa na miezi 6 unaweza kumuuza kwa elf 10,000-hadi 15,000 na changamoto zake sio kubwa wanakula masaa 12 tu per day usiku sio lazima sana kuwapa chakula.

Unaweza kuwapa chakula cha kiwandani mfuko mmoja kama Start tu kwani katika kipindi cha siku 0 hadi 30 wanatakiwa wapate chakula ambacho the best kwa ukuaji pia sio-lazima unaweza kutengeneza mwenyewe Start unaweza ku-Google Fromula za chakuala.

Baada ya kipindi cha siku 30 unaweza kuwapa mapumba na mboga mboga kwa wingi na wakakua kwa speed ya ajabu zingatia sana usafi wa vyombo nk.... Mapumba kilo 200 kuhu kwetu so kama upo serious unaweza ukalima mwenyewe mahidi ukaweka hala la mapumba.

Chakula cha kuku wa Broiles uwezi kutengeneza mwenye kwasababu kama kukitokea stuetion ya vitam kupungua hawakui hawanadumaa tu. lazima kipitie maabala kipimwe.

Ushauli: kama unataka kupiga pesa vizur fanya project zote kwa pamoja

[I mean fuga kuku chotala kwaajili ya kuwauza nyama na fuga kuku wa broilers. Ukimudu vizur kusimamia faida utaipata kubwa.]

Naomba niishie hapa.
 
[I meana fuga kuku chotala kwaajili ya kuwauza nyama na fuga kuku wa broilers. Ukimudu vizur kusimamia faida utaipata kubwa.]

Naomba niishie hapa.
Ahsante kwa ushauri chief nitaufanyia kazi.
 
Mchango wako pia muhimu mkuu kama una experience na ufugaji.
angalia kama una mtaji wa uhakika. Maana kroiler kwenye kula aisee usipoangalia utawauza kabla hawajafikia malengo yako.
Hii ni kwasbb kroiler wanakaa mda mrefu mpka kuja kuuza kuliko broiler.

Kwenye upande wa broiler hawa ni mda mchache na kama mdau alivyosema hapo kawaida faida yao huwa 1000- 1500 kwa kuku mmoja.

Nliwah kuona mfugaji wa kroiler alikuwa nao 100 walikuwa wanamaliza gunia la kilo 100 la chakula kwa wiki mbili tu mda mwngne hta wiki mbili zinaweza zisifike.

Kroiler wana faida ila kabla ya kupata hyo faida lazima uwe umejipanga mtaji.
 
Back
Top Bottom