Naombeni msaada wakuu

ndugu yako

Senior Member
Joined
Mar 30, 2013
Posts
193
Reaction score
96
habari zenu wakuu wa jukwaa hili!
wanabodi naomba msaada wenu katika kunisaidia kujibu haya maswali yangu!
[TABLE="width: 500"]
[TR]
[TD]1) je ni kweli kuwa kama kampuni ikianzishwa na watu wawili au zaidi, waanzilishi wa hiyo kampuni hawawezi kuwa na hisa sawa?! mfano, nimeambiwa eti kwenye kampuni ambayo imeanzishwa na watu wawili haiwezekani wote kuwa na hisa kiwango sawa yan asilimia 50 kwa 50 au asilimia 45 kwa 45, ila kinachowezekana ni mmoja kuwa na hisa nyingi zaidi ya mwingine yani inapaswa kuwa walau asilimia 50 kwa 40?!

2) je million tano zinatosha kuwa mtaji wa kuanzisha kampuni?!

3) je mtu anaweza kuanzisha kampuni (officially) bila ya kuwa na phyiscal office?!

4) kwa kampuni inayoanza na mtaji wa millon 5 Tsh. inatakiwa kulipa kodi asilimia ngapi?!
b) kodi inalipwa mwanzoni kampuni inapofunguliwa au inalipwa kutokana na faida kampuni iliyopata?!

5)kwa kuanzisha kampuni ambayo kwa kuanzia itakuwa ina deal na uwekezaji mdogo mdogo mfano kuwekeza katika soko la hisa, kuwekeza katika public transport like daladala, natakiwa niwe na leseni ngapi na za aina gani?!
b) bei ya leseni kwa hapa Tanzania ni kiasi gani?
[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
1. Sina hakika ni nani amekwambia hivyo, lakini share capital (mtaji) unaweza kugawanywa kwa ratio ya 50:50.

2. Share capital ya kampuni haijalishi kama una kiasi kikubwa au la. Kinachotakiwa uwe na idadi ya hisa na thamani yake, na hao shareholders wanatakiwa wachukue baadhi ya hisa na kuzilipia kwa kiasi kile wanachoweza.

Unaweza kuanzisha kampuni kwa issued share capital ya laki tatu achilia mbali milioni tano!

3. Physical office kwa Tanzania huwa kama ni lazima vile. Lakini kwa kuaznia unaweza kutoa address ya nyumbani kwenu au kwako sio lazima ukakodi mlango Posta au Kariakoo.

4. Kodi inategemea na aina ya biashara utakayofanya. Wanachotaka TRA mara nyingi kwa baadhi ya biashara ni kufanya estimate ya mapato yako kwa mwaka kabla ya kuanza kufanya biashara yenyewe na kulipia kiasi fulani kama kodi ambayo ni 30 percent ya net income.

5. Leseni siku hizi nafikiri ni bure ukisha kuwa na documents zote halali zinazohitaji.

Kila biashara ina leseni yake nafikiri. Lesini ya dala dala haiwezi kukuruhusu kuwa agent at the same time kwenye soko la hisa!

Mtafute mwanasheria wa kawaida tu anaweza kukusaidia kusolve hizi issues. Ni mambo madogo mno!
 
shukrani mkuu kwa kunipa mwanga!
kuhusu hyo share capital kuna mtu (ambaye nataka nishirikiane naye kwenye biashara) aliniambia kuwa eti hayo ni matwakwa ya sheria!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…