Mimi ni kijana nimemaliza degree ya sheria miaka minne chuo cha RUCO Iringa 2011, nimeangaika sana kutafuta hata sehemu ya kujiatachi nimekosa kabisa, kutokana na kipato kidogo cha familia yetu nimeshindwa kuendelea na Law school, ila kuna wasamaria wema wamenisikia wananisaidia nikasome MASTERS wamenishauri nibadilishe fani kidogo nikachukue MBA au MASTERS ya HR, ili niendane naushindani wa soko la ajira hapa Tanzania, nisaidieni wana JF nikasome ipi iniwekwe kwenye ajira umri nao unaenda kwa speed sana.
ushauri wangu mimi ni"one step at a time"nafikiri ni vema hatua ya kwanza ukaimaliza.Nenda law school , ukiisha maliza tafuta chamber ujiegeshe,Mungu akituweka hai ,naweza kukuombea ,nnajamaa zangu wengi wamefungua hizi.Upige pilikapilika za mjini,huku ukifanya test zenu za u advocate,then baadae ndio uone kama utahitaji kusoma hizo masters.sikushauri sana kusoma kwa kuruka ruka.Malizia kwanza hiyo misingi ya kisheria.
Lakini pia jambo la msingi ni kupata uzoefu kwanza,kazi za siku hizi ukiwa fresh zinakua ngumu sana.Ukimaliza Law school nadhani itakusaidia pa kuanzia.Masters unaweza kuja kujisomesha.
dogo jaribu kupita hapa PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT - PSRSMimi ni kijana nimemaliza degree ya sheria miaka minne chuo cha RUCO Iringa 2011, nimeangaika sana kutafuta hata sehemu ya kujiatachi nimekosa kabisa, kutokana na kipato kidogo cha familia yetu nimeshindwa kuendelea na Law school, ila kuna wasamaria wema wamenisikia wananisaidia nikasome MASTERS wamenishauri nibadilishe fani kidogo nikachukue MBA au MASTERS ya HR, ili niendane naushindani wa soko la ajira hapa Tanzania, nisaidieni wana JF nikasome ipi iniwekwe kwenye ajira umri nao unaenda kwa speed sana.
Jaribu kuumiza kichwa sana kuhusu kujiajiri na si kuajiriwa. Elimu uliyo nayo ni kubwa sana kukuwezesha kujiajiri. Jipange vizuri. Pia kaa ukifahamu ajira nyingi sana zinaenda kwa kuwa na connection, elimu kubwa ya masters unaweza kupata na bado ukasugua kitaa!
Huko kutakuwa serikalini, ndo maana ufanisi huko mbovu wakati kampuni kama toyota, sony zinazidi kuitingisha dunia kwa mafanikio. Watu wanataka ufanisi sio vyeti vingi
nakushauri ukae chini na kufikiria biashara ya kufanya kwa mtaji wa hiyo school fees ya masters, waambie wakupe mkonon ujaribu ujasiriamali as kusoma masters hakuna msaada wowote kwenye soko la ajira nowdays masters sio ishu tena watu wanasugua kitaaa mpaka wanajuta
I will differ with you slightly, ukiangalia hizo kampuni umezitaja hapo, nenda angalia their R&D departmet you will be shocked to find how many Phd holders wako huko. Dunia ya leo research ndio insababisha kampuni inatick!
Research and development centre ni heart ya kila kampuni as new product developments, market, zinaanzia huko but I am talking about key peoples... Nitajie kampuni ya tanzania yenye research and development centre serious itayotuajiri tukiwa na hizo phd na kutulipa vizuri..
Wapi serikalin kuna research and development centre serious yenye ufanisi as sony, huawei, samsung..
Mpaka leo kampuni za kiafrika zimeshindwa kufanikiwa kwa poor recruitment and promotion programes based on certificates etc as operations companies like tanesco lazima zi base kwenye perfomance as mnauza service to customers,, hebu imagine kampuni kama Tanesco inavyosua sua wakati ni monopoly as kila mtanzania ni mteja wake, ina wateja maelfu lakini inashindwa kujiendesha wakati almost all of senior managers, head of departments wana masters etc,,,
Wenzetu wanaweka watu wa shule katika position zinazihitaji shule tu as research and development centre, but kwenye sehem za operations experience and performance ndo inakuwa considered kumchagua mtu and not certificates.
Kwa style hii haitawezekana hata tukizaliwa upya kwa Tanzania kuja kuwa na kampuni levo za Toyota, Nokia etc as huko hakuna longo longo za vyeti tu, kazi zinafanywa kwa ku meet target as ukizembea tu Competitor anakupora customers.. Angalia presha walio nayo Apple, Samsung, Htc, Huawei, Nokia katika kugombania wateja ndo utajua why key peoples hawana elimu kubwa sana lakini experience za kufa mtu