Naombeni msaada wenu wakimawazo wanajf wenzangu....... Ndugu hawa

Naombeni msaada wenu wakimawazo wanajf wenzangu....... Ndugu hawa

sharobaby

Member
Joined
Apr 8, 2011
Posts
69
Reaction score
10
last three months nilipatwa na msiba baba yangu kipenzi, tukazika salama na kila kitu kimeenda vizuri hakukuwa na tatizo lolote..about two weeks sasa yamenza kubumburuka mambo ya nani mrithi wa marehemu...mzee ameacha mtoto mmoja ambaye ndio mimi ninaye andika hii thread na mke ambaye ndio mama yangu mzazi, kiukweli mzee hakuwa na mali za hivyo amecha nyumba yake moja ya kawaida tu na shamba moja na kagari ...sasa kuna baba yangu mkubwa mmoja amenza kusema kwakuwa marehemu ameacha mtoto wa kike basi lazima arithi na ndugu mmoja wa kiume na akapendekeza mwanawe ndio awe mrithi na blaa blaa kibao ...sasa jamani wanaJf wenzangu hii imekaaje
 
imekaa vibaya!!!!!!!!

huyo mwanawe mali za baba yako zinamhusu kitugani????????

kwanza ww unaonaje maana naona kama mwenyewe umeridhika then unatutega tu!!

waswahili husema jina la kitu ni kitu chenyewe, Sharobabby acha mambo ya usharo kwenye mali za baba yako hali yakwamba unajielewa!!!

Ila pole kwa msiba.
 
Tafuta mwanasheria maana huyo mzee anachotaka ni kuwakaba kabari huku mkiona!
 
anatumia mila za kabila gani huyo babako mkubwa?... ukinitajia kabila nitafuatilia mila ila navyojua mie ..MILA NYINGI ZA KIAFRIKA mama yako angerithiwa na babako mdogo/mkubwa kisha "kama watazaa" mtoto wa kiume then hilo tunda la ndoa ya urithi ndio atakuwa mrithi...hiyo ilikuwa ikitumika sanaa enzi za ujima ila sikuhizi imekwisha...

mwambie huyo dingi yako kuwa marehemu mshua wako nilikuwa namdai tshs 1billion kwa hiyo auze mali za marehemu babako na mali zake yeye na ndugu wengine "WANILIPE PESA ZANGU NISEPE"...wakikubali hilo deni langu waambie na wewe umekubali mwanae arithi jasho la babako...

UMENIELEWA?...MWISHO NAKUPA POLE YA KUPOTELEWA NA MSHUA WAKO...MAAANA NAJUA ANGEKUWEPO PANGECHIMBIKA.
 
Kisheria Mama Huyo baba yako na hao wanae awatakiwi kugusa hata sent moja ya marehemu baba yako kwani binadamu wote ni sawa na hakuna wa kike au wa kiume wote ni watoto hivyo hata wewe ni mtoto na unatakiwa kurithi mali zote za marehemu baba yako. Habari ndio hiyo na wakileta ujinga nenda TAMWA wakupe msaada wa kisheria mama. Choa have a ni day wasikupe presha mtoto wa kike tulia.
 
Hilo jina nalo kiboko...................

Umenikumbusha kisa kimoja cha mali za marehemu shem wangu alifariki akaacha nyumba, gari na mashamba (mkewe pia alikuwa ameshafariki) hata kuzikwa alikuwa bado Baba mdogo akaanza kusema gari nitachukua mimi na nyumba nachukua mimi ili nilee watoto wa marehemu (wawili) bwana wewe ule msemo wa kuwa kuna watu huondoka na vitu vyao duniani ulitimia baada ya kuzika na kuanza vikao vya mali hamadi wakati wanachukua nguo za kwenda kumaliza msiba home (kijijini) walichokiona walikoma nacho kila kitu kauza ndani ya wiki mbili walichoambulia ni milioni sita tu ndo walikuta ndani.

Pole sana haya mambo yapo sana ila kuwa ngangari kama vipi mshauri mama uza gari nunua lingine
 
sharobaby leo umenikumbusha mshua alivyovuta wakataka kuanza kuongelea mali za mshua si tukawawahi na kuwaambia tupo watoto 7 mshua kaacha nyumba moja na mengineyo..sasa ndugu tunaomba muhakikishe kila kijana wa marehemu anapata urithi wa nyumba 1... TUCHANGIENI VIJANA WA MAREHEMU NYUMBA 6 ZA KUGAWANA WATOTO WA MAREHEMU....kikao kilifungwa kila-mtu alitoroka...tukamwambia mjane aka bi mkubwa wetu tuchape lapa tumewatuliza na hawatorudia ujinga... MWAMBIE BABAKO MKUBWA ARITHI NA MADENI YA MAREHEMUU MSHUA KWA HIYO AUZE NYUMBA YAKE NA MENGINEYO MLIPIE DENI LA MAREHEMU....UTAWAONA WATAVYOPOTEANA NA MJADALA KUFA KIBUDU
 
Pole, cha kukushauri we na mama yako komaeni nae kama ni undugu uishe, hawana haya. tamwa wapo, haki za binadamu wapo, na sheria ipo
 
Nigee namba ya dingi yako mkubwa nimchane aache mambo ya ki-kale karne hii... Au nimlipue ajute kuja na mawazo ya kipuuzi...mwambie ms@#%%^#$#enge mkubwa
 
Sharobaby nakushauri kitu kimoja cha msingi tena fanya haraka wala usifanye mzaha nenda kawaone TAMWA uwaeleze kila kitu ukihitaji msaada wa jinsi ya kufika huko nishtue i will direct you ili ukawaone
 
  • Thanks
Reactions: BAK
1st of all POLE SANA,
Ukikomaa kama wachangiaji walivyosema hawatagusa chochote,
Kitu cha kufanya nenda mahakamani uwe msimamizi wa mali za babako.
Hadi lini sisi wabongo tuataacha haka ka mchezo, pindi nduguyo anapokufa unakimbilia mali Wakati anazitafuta ulikuwa wapi?
Kila mtu akarithi vya babake, tena ni baba mkubwa inasikitisha sana.
Wakati mwingine ukikaa na kufikiri unaweza kudhani watu huwa wanaombea mtu afe ili aje warithi.
NCHI INAKUWA MASIKINI KWA TABIA YA KUPENDA VYA ULAINI.
MWENZENU APINDE MGONGO, TENA YAWEZEKANA ALIWASAIDIA LAKINI HAMSAIDIKIKI, ILA MACHO KODO KWENYE MALI ZAKE.
YALISHANIKUTA, SO NINAUJUA UCHUNGU ULIONAO BUT AT THE END OF DAY UTAWASHIDA NA UTAMJUA NANI NI NDUGU WA KWELI.
POLE SANA
 
Poleni sana yaani ndugu wao huwa wanasubiri mtu afe waanze kugombea mali kwanini wao hawatafuti kwa jasho?
 
last three months nilipatwa na msiba baba yangu kipenzi, tukazika salama na kila kitu kimeenda vizuri hakukuwa na tatizo lolote..about two weeks sasa yamenza kubumburuka mambo ya nani mrithi wa marehemu...mzee ameacha mtoto mmoja ambaye ndio mimi ninaye andika hii thread na mke ambaye ndio mama yangu mzazi, kiukweli mzee hakuwa na mali za hivyo amecha nyumba yake moja ya kawaida tu na shamba moja na kagari ...sasa kuna baba yangu mkubwa mmoja amenza kusema kwakuwa marehemu ameacha mtoto wa kike basi lazima arithi na ndugu mmoja wa kiume na akapendekeza mwanawe ndio awe mrithi na blaa blaa kibao ...sasa jamani wanaJf wenzangu hii imekaaje

Pole saana dear kupotelewa na baba yako. Kama tayari umri wako ni 18 na zaidi, huna la kuhofia mana kama uko chini ya umri issue inakua kua who is your guardian. Hata hivyo we kwa sasa kurithi hizo mali chache (kama ulivyosema) sidhani hata kama kuna la kujali hapa, sidhani kama watakuja kumnyanga'nya mamako na kumfukuza hapo home; after all i believe yeye ndo mrithi kwa sasa.
 
Huyo nae ba mkubwa wako wazamani kweli? hivi siku hizi bado watu wanatolea macho mali za ndugu zao wakati kuna mke na watoto? usikubali kabisa tafuta mwanasheria umtoe baru
 
last three months nilipatwa na msiba baba yangu kipenzi, tukazika salama na kila kitu kimeenda vizuri hakukuwa na tatizo lolote..about two weeks sasa yamenza kubumburuka mambo ya nani mrithi wa marehemu...mzee ameacha mtoto mmoja ambaye ndio mimi ninaye andika hii thread na mke ambaye ndio mama yangu mzazi, kiukweli mzee hakuwa na mali za hivyo amecha nyumba yake moja ya kawaida tu na shamba moja na kagari ...sasa kuna baba yangu mkubwa mmoja amenza kusema kwakuwa marehemu ameacha mtoto wa kike basi lazima arithi na ndugu mmoja wa kiume na akapendekeza mwanawe ndio awe mrithi na blaa blaa kibao ...sasa jamani wanaJf wenzangu hii imekaaje

Ee Mungu wangu ee!...haya mambo na ujinga huu utaisha lini yarabi?
Mzee wako hakuacha wosia?

Kwakweli inabidi tu kuchukua msaada wa kisheria.
Bahati mbaya, mambo ya urithi hupelekea uhasama mkubwa wa wanandugu,
lakini huna budi kufanya hivyo kwa faida ya Mama yako, na yako binafsi na uzao wako.

Pole sana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Pole sana kwa msiba mkubwa uliowafika wa kuondokewa na Baba yako. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Hayo mambo ya kizamani kwamba mtoto wa kike hastahili kurithi mali ya wazazi wake. Hakuna yeyote mwingine mwenye haki na mali ya marehemu ila wewe na mama yako. Msikubali kudhulumiwa chochote kile katika mali alizoziacha marehemu. Pole sana.
 
Pole sana Sharobaby, cha msingi jitahidi uwe msimamizi wa mirathi au mama yako, achana kabisa na huyo baba yako mkubwa tena ni jambazi kabisa, kama yeye atakubali arithiwe hivyo, hata uchungu wa mali kwanza haujui.
 
susy my dia ningekuwa nimeridhika na hilo nisingelileta hapa jaman...mi mwenyewe nashindwa kumuelewa huyo mtoto wake zinamuhusu nini naamemchagua yeye mwenyewe na anatake adnantage kwa sababu yeye ndio mkubwa wao..

Back
Top Bottom