last three months nilipatwa na msiba baba yangu kipenzi, tukazika salama na kila kitu kimeenda vizuri hakukuwa na tatizo lolote..about two weeks sasa yamenza kubumburuka mambo ya nani mrithi wa marehemu...mzee ameacha mtoto mmoja ambaye ndio mimi ninaye andika hii thread na mke ambaye ndio mama yangu mzazi, kiukweli mzee hakuwa na mali za hivyo amecha nyumba yake moja ya kawaida tu na shamba moja na kagari ...sasa kuna baba yangu mkubwa mmoja amenza kusema kwakuwa marehemu ameacha mtoto wa kike basi lazima arithi na ndugu mmoja wa kiume na akapendekeza mwanawe ndio awe mrithi na blaa blaa kibao ...sasa jamani wanaJf wenzangu hii imekaaje
Dada yangu Sharobaby
Kisheria kuna vitu 2 hapa vinahusika. Kwa kuanzia inategemea mambo 2 makubwa:
(i) Kama baba alifariki akaacha wosia (if he died testate)
(ii) Kama hakuacha wosia (if he died intestate).
Kama aliacha wosia wa namna mali zigawanywe basi huo utafuatwa kama ulivyo na kama baba mdogo anakwenda kinyume anabanwa na sheria. Wosia humtaja msimamizi wa mirathi ambaye LAZIMA afuate matakwa ya marehemu kama yalivyo. Akikiuka anashtakiwa mahakamani. Hii ni njia rahisi sana ya kuepusha migogoro baada ya kifo. Lakini sidhani kwa case yako kama mzee aliacha wosia.
Kama hakuacha wosia mahakama ndiyo inayohusika na kumthibitisha msimamizi wa mirathi (administrator au administratix kulingana na jinsia yake). Hufanya hivi
baada ya kikao cha ukoo (ndugu) kukaa na kufikia makubaliano nani awe msimamizi wa mirathi. Kumbukumbu (minutes) za kikao hiki
LAZIMA hupelekwa mahakamani ambayo
humthibitisha au kutengua uteuzi huo. Kwa kawaida kama wewe au mama hamkuridhika na uteuzi wa kikao cha ndugu mnaweka
pingamizi mahakama isimthibitishe huyo aliyeteuliwa. Mathalani, mama au watoto ndiye ana haki ya kwanza kuwa msimamizi wa mirathi hiyo kama wameshafikia umri wa utu uzima kisheria. Hivyo kama wewe ni mkubwa unaweza kuwa msimamizi au mama. Lakini ukiwa wewe kumbuka utabanwa na sheria kuhusu namna ya kutumia hizo mali kwa ajili ya mama -mjane wa marehemu. Sio unaanza kutapanya. Baba mkubwa pia anaweza kuteuliwa kulingana na mazingira ya familia yenu na kama nyie mmeridhika. Akishathibitishwa mahakama hutoa maelekezo ya namna ya kusimamia mali hizi (hapa ni pamoja na kupewa jukumu la kuainisha na kubainisha mali zote, mahali zilipo na thamani yake). Haruhusiwi msimamizi wa mirathi kufanya kinyume na hayo au kuzitumia mali hizo kwa ajili yake. Ni kosa na akifanya hivyo mahakama itatengua usimamizi wake pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kama baba alikuwa anaishi maisha ya kiislamu kuna pia taratibu za kiislamu kuhusu mirathi ambazo zinafuatwa na sheria inazitambua. NB Kuwa tu muislamu kwa dini au jina haitoshi kuwa aliishi kiislamu. Hii inategemea namna "alivyoendesha maisha yake"-je aliincline kwa mirathi ya uislamu au la? Mara nyingi watu ni waislamu lkn mfumo wa maisha yao unaathiria kuwa walipenda mirathi ya sheria ya nchi itumike.
Pia kama aliishi maisha ya kitamaduni sana (ambayo sidhani kama tz wapo tena wengi) basi utaratibu wa customary succession utatumika. NB Utaratibu huu lazima uwe hauvunji sheria za nchi-hasa katiba. Kama kimila mwanamke haruhusiwi kabisa kurithi mali hiyo haiwezi kukubaliwa.
Conclusion.
Kwa maelezo yako nadhani zile namna 2 nilizoeleza pale juu ndio zinaapply kwenu. Kuhusu testate or intestate succession. So, cha msingi muende mahakamani (mahakama ya mwanzo tu inatosha) mfungue shauri la mirathi. NB
Hii sio kesi bali ni maombi ya mahakama iwatangaze mmoja wenu (mama hususan) kama msimamizi wa mirathi. Msiogope kwani hapa sio kwamba mnamshtaki baba mkubwa. Mkishampata huyo mtakuwa mmeshakwepa huyo mroho. Huko TAMWA na kwingine hata ukienda watakupaleka ktk utaratibu huu.
Natumaini nimekupa mwanga.
Asante.