Ndugu Bakarikazinja;
Nimesoma ujumbe wako, mara kadhaa kwa siku tofauti leo ndo nimeona niandike ushauri wangu, kwani naona hakuna aloandika, ni hivi;
Tafuta sehemu ambayo utajitolea au utatumia kipaji chako bure (bila kulipwa), au kwa malipo kidogo yasilingana na ujuzi wako), kwani naona tatizo lako ni kuwa huna umjuaye alokuwa anga zinanazofaa (tatizo la Tz ni kuwa siyo kuwa unajuwa nini bali unamjua nani), hivyo inabidi ujitangaze mwenyewe. Mfano, tafuta gazeti uwe unatoa nakala bila hata kulipwa, au tafuta shule uwe unaenda kufundisha walimu au wanafunzi hata kama ni saa moja kwa wiki. Au tafuta Taasisi isiyo iliyo au isiyo ya kiserikali ambayo inaweza kuwa inahitaji utaalam wako, lakini hawawezi kukulipa uwe unajitolea tolea huko. (ukiona vipi ni PM au email ili nikueleweshe zaidi)