Naombeni msaada wenu

Naombeni msaada wenu

bakarikazinja

Senior Member
Joined
Nov 9, 2009
Posts
177
Reaction score
8
Mimi nina kipaji kizuri cha kuandika kazi za fasihii nimesomea kazi za ubunifu university of dar es salaama lakini sijui nifanyeje ili nikiendeleze kipaji changu kwani nina mengi moyoni ila kupitia hizi kazi ndio na weza kuyatoa hadharani
 
Kama hujui ufanyeje huku unatambua kwamba una kipaji basi nenda ukalale kwa kuwa hujui chochote!
 
Kama hujui ufanyeje huku unatambua kwamba una kipaji basi nenda ukalale kwa kuwa hujui chochote!
mkuu si umshauli tuuu kama huna la kusema tulia, wacha wanyemichango yao watoe!
 
Asante sana henge maana sababu moja wapo ya kujiunga na jamvi ni kupata ushauri na ndio maana nipo humu hivyo naomba unishauri na siyo kunitukana
 
Hongera kwa kuwa mbunifu, naamini baada ya kitambo kidogo utabuni namna ya kuendeleza kipaji chako, ndiyo maana zawo la wasomi ni kubuni na kutafiti ili kutatua adha zinazotukabili kijamii. chonde usijiunge na vikundi vya mafisadi kwa mafanikiyo ya chapuchapu. upo hapo!:msela:
 
Andika kazi zako, kama ni hadithi, michezo ya kuigiza au mashairi, badaye tafuta shirika la kuchapisha. Ikiwa ni za kielimu unaweza kupeleka Oxford University Press.
HATUA YA MWANZO: KUSNYA KAZI ZAKO NA KUANDIKA.
Usivunjike moyo
 
asante mama mia nitafanya kama ulivyo ni shauri ila hawa oxford university press sijui wako wapi ?ila na shukuru sana
 
Kaka, UDSM, pale Taasisi ya Taaluma za Kiswahili(zamani TUKI) kuna Idara ya Fasihi, Maandishi na Uchapishaji. Hebu fika uwaone wahusika, nadhani unaweza kupata msaada pale.
 
asante mama mia nitafanya kama ulivyo ni shauri ila hawa oxford university press sijui wako wapi ?ila na shukuru sana

Wako pale Mikocheni B, shuka kituo cha pili mbele ya hicho cha B, kama unatokea Kawe, vuka barabara, utaona jengo la CCM, uliza wadau Oxford ni wapi, watakuelekeza.
 
Onana na shingogo akupatie DVD ya Streat Univercity utajua namna ya kutoka kimaisha kwani uliyosoma UDSM hakuna kitu , ulitumia muda na karo ya wazazi bure.
 
Onana na shingogo akupatie DVD ya Streat Univercity utajua namna ya kutoka kimaisha kwani uliyosoma UDSM hakuna kitu , ulitumia muda na karo ya wazazi bure.

Jamani usikiponde hivyo chuo chetu - bila justification yoyote.
 
Mkuu kama una kipaji tafuta compyuta aanza kuandika na washirikishe watu then chapisha nawe utatoka
 
asante mama mia nitafanya kama ulivyo ni shauri ila hawa oxford university press sijui wako wapi ?ila na shukuru sana
Nilitaka kukuelekeza wapi ipo Oxford University Press, lakini naona tayari umeshaelekezwa. Fuata ushauri huo uliopewa wa kuziandika kwa Compyuta. Ukiwa tayari wasiliana nami nikuelekeza kwa mtu ninayemjua hapo OUP.
KIla la heri.

Ah! Amgalia kwenye maandishi mekundu. Jina langu hapa ni Mammamia, lote pamoja na "double m" na sio mama mia.
 
Ah, just id tu bana, muhimu kuelewana.
 
Mtafute mtu mmoja anaitwa babalao anapatikana humuhumu jamvini, binafsi simjui ila anadai kuwa anasaidia watu kwenye mambo kama hayo
 
asante sana wanajamvi yaani kwa ushirikiano mlionipa naona kama vile mbele yangu kuna mwanga fulani yaani sijui siku zote nilikuwapi kujiunga na jamii forum
 
Ndugu Bakarikazinja;

Nimesoma ujumbe wako, mara kadhaa kwa siku tofauti leo ndo nimeona niandike ushauri wangu, kwani naona hakuna aloandika, ni hivi;

Tafuta sehemu ambayo utajitolea au utatumia kipaji chako bure (bila kulipwa), au kwa malipo kidogo yasilingana na ujuzi wako), kwani naona tatizo lako ni kuwa huna umjuaye alokuwa anga zinanazofaa (tatizo la Tz ni kuwa siyo kuwa unajuwa nini bali unamjua nani), hivyo inabidi ujitangaze mwenyewe. Mfano, tafuta gazeti uwe unatoa nakala bila hata kulipwa, au tafuta shule uwe unaenda kufundisha walimu au wanafunzi hata kama ni saa moja kwa wiki. Au tafuta Taasisi isiyo iliyo au isiyo ya kiserikali ambayo inaweza kuwa inahitaji utaalam wako, lakini hawawezi kukulipa uwe unajitolea tolea huko. (ukiona vipi ni PM au email ili nikueleweshe zaidi)
 
Back
Top Bottom