Naombeni Msaada, WIFI adapter ipi iko vizuri kwenye computer?

Mr_Plan

Senior Member
Joined
Oct 2, 2021
Posts
140
Reaction score
194
Habari Wanajamvi Natumai ni wazima wa Afya....Nilikuwa naomba kufahamishwa Je ni Wifi Adapter ipi ambayo naweza Tumia kwenye Computer bila Tatizo na Yenye kasi zaidi.

 
Computer aina gani
Desktop au laptop?

Dlink wireless adapters tafuta ni nzuri.
 
Duuuu.....🤣🤣🤣 Si Uulize kama Uelewi
 
ndio ivyoivyo wala ujakosea
 
Mimi nataka kuitumia kwenye desktop. Je washauri ninunue ipi
Tafuta za Pcie ambazo Unachomeka ndani ya desktop zina Bluetooth Na wifi humo humo zipo kama hivi



Za wifi 5 minimum ni kama 20,000-30,000 Aliexpress mpaka ina kufikia na za wifi 6 ni kama 40,000-50,000.

Kwa matumizi ya kawaida Wifi 5 inatosha hata router zetu nyingi kibongo bongo zinaishia hapo ila kama unataka future proof chukua ya wifi 6.
 
Umesema nikwamatumizi ya kawaida wifi 5 na je wifi 6 ni kwamatumizi gani labda?

Na kama mtu ana laptop ni adapter gani unam recommend, maana nataka ku install parrot os sasa nataka nijaribu hacking moja ya wifi.
 
Umesema nikwamatumizi ya kawaida wifi 5 na je wifi 6 ni kwamatumizi gani labda?

Na kama mtu ana laptop ni adapter gani unam recommend, maana nataka ku install parrot os sasa nataka nijaribu hacking moja ya wifi.
Wifi 6 ina speed zaidi kama unacheza games, una stream na kufanya kazi nzito inahitajika.

Laptop nunua wifi za M2 za intel zipo kama hivi.


Sema angalia kwanza laptop yako inakubali mfumo upi, M2, msata Etc ununue according to mfumo wako.
 
Tofauti ya hiyo na hii iko wapi mkuu sina idea kwenye hili
 

Attachments

  • Screenshot_2023-11-20-09-31-53-092_com.opera.mini.native.jpg
    97.5 KB · Views: 4
Tofauti ya hiyo na hii iko wapi mkuu sina idea kwenye hili
Hii inachomekwa kwenye usb ambayo ni slow, theoretical usb 2.0 haizidi 480mbps (60MBps), wakati zile nilizokutajia zinatumia Pcie ama M2 ambazo ni 64Gbps ama zaidi. Pia hizi nyingi ni wifi 4 kushuka pcie nilizokuekea ni wifi 5/6

Pia ubora, hivi mara kwa mara vinakufa, vile ni intel unakaa navyo hadi unasahau.
 
Hapo shukrani nmekuelewa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…